Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia agoma kuingilia sakata la kina Mdee
Habari za Siasa

Rais Samia agoma kuingilia sakata la kina Mdee

Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan, amekataa kukubali ombi la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuingilia kati sakatala la wabunge viti maalum 19, wanaodaiwa kuwepo bungeni kinyume cha sheria, akisema suala hilo liko mahakamani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro … (endelea).

Msimamo huo wa Rais Samia ulitolewa leo tarehe 8 Machi 2023, akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Kilimanjaro, yaliyoandaliwa na Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha).

Ni baada ya baraza hilo na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, kumuomba aingilie kati ili wabunge hao waondolewe bungeni kwa madai kuwa hakijawateua.

“La mwisho kwa jina mliloliita (Covid-19), wote wawili wamesema japo kwamba lipo mahakamani lakini mama…, niwaambie tuache mkondo ule uendelee tutazame mbele yanayokuja. Tuachie mkondo ule uendelee, si rahisi mimi hata kama ni Rais kutia mkono huko,” amesema Rais Samia.

https://www.youtube.com/watch?v=RtdYO5O0tXk&t=33s

Wabunge hao wakiongozwa na Halima Mdee, walifungua kesi Na. 36/2022 katika Mahakama Kuu, Masjala Kuu, jijini Dar es Salaam, kupinga uamuzi wa Chadema kuwavua uanachama kwa tuhuma za usaliti kufuatia uamuzi wao wa kwenda kuapishwa bungeni jijini Dodoma, kuwa wabunge viti maalum.

Katika kesi hiyo inayosikiliwa mbele ya Jaji Cyprina Mkeha, Mdee na wenzake wanadai hawakujipeleka bungeni, bali waliteuliwa na uongozi wa chama hicho, hivyo wanaiomba mahakama ifanye mapitio dhidi ya mchakato uliotumika kuwavua uanachama wakidai haukuwa halali.

Kwa sasa kesi hiyo inaendelea kusikilizwa mahakamani hapo, ambapo kesho tarehe 9 Machi 2023, mawakili wao wataanza kuwahoji baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wadhamini la Chadema, akiwemo Dk. Azaveli Lwaitama, dhidi ya hati zao za viapo kinzani walizowasilisha mahakamani kujibu malalamiko ya wabunge hao kufukuzwa kinyume cha sheria.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!