RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa wenyeviti wanne wa Bodi za Wakurugenzi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Taarifa iliyotolewa na Jaffar Haniu, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu imesema, uteuzi wa wenyeviti hao, umefanyika leo Jumatano, tarehe 16 Juni 2021.
Amewataja walioteuliwa ni;
1. Juma Alli Mohamed Muhimbi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Kabla ya uteuzi huo, Muhimbi alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Transparent Finacial and Tax Consulting Services Ltd ya Dar es Salaam.
Muhimbi anachukua nafasi ya Mama Anne Makinda, Spika mstaafu wa Bunge la Tanzania, ambaye muda wake umemalizika.
2. Amemteua Dk. EdmundMndolwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB).
Dk. Mndolwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), anaendelea na wadhifa huo baada ya kumaliza kipindi chake cha kwanza.
3. Amemteua Prof. John Wajanga Aron Kondoro kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC).
Prof. Kondoro anaendelea na wadhifa huo baada ya kumaliza kipindi chake cha kwanza.
4. Aidha, Rais Samia amemteua Prof. Valerian Cosmas Kanyengele Silayo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC).
Prof. Silayo ni Profesa wa Chuo Kikuu cha Kilimo Morogoro (SUA).
Hiyo headline ina utata
Ni kama vile Makinda ameteuliwa. Mnababisha