RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali. Anaripoti Nasra Bakari, DMC … (endelea).
Uteuzi huo, umetangazwa jana Alhamisi, tarehe 22 Aprili 2021 na Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu.
Walioteuliwa ni;
1. Amemteua Prof. Henry Fatael Mahoo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.
2. Amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufani, Dk. Gerald Ndika kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.
Dk. Ndika ameteuliwa kushika wadhifa huo kwa kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwanza kumalizika.
3. Amemteua Prof. Aurelia K. Kamuzora kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kahawa Tanzania.
4. Amemteua Prof. Idris S. Kikula kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini Tanzania.
Prof. Kikula ameteuliwa kushika wadhifa huo kwa kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwanza kumalizika.
Msigwa amesema, Rais Samia amewateua Prof. Abdulkarim Mruma na Janeth Lekashingo kuwa wajumbe wa Tume ya Madini Tanzania.
Uteuzi wa viongozi hawa umeanza tarehe 20 Aprili, 2021.
Leave a comment