October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia aeleza sababu ya kuzindulia Royal Tour Marekani

Spread the love

 

RAIS Samia haikuwa bahati mbaya kuzindulia filamu ya kutangaza utalii wa Tanzania duniani, Royal Tour nchini Marekani bali ni kutokana na nchi hiyo kuwa makazi ya watu wengi wanaopendelea burudani na starehe. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Amesema hayo leo Ijumaa ya tarehe 15 Aprili 2022 alipokuwa akizungumza na Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris na mbele ya wanahabari katika Ikulu ya White House Washington DC nchini Marekani.

Katika video iliyorushwa kwenye chaneli ya YouTube ya Ikulu, Rais Samia amesema, “Kuichagua Marekani kwaajili ya uzinduzi haikuwa kwa bahati mbaya tanatambua na tumefanya kwa makusudi kwa kujua kwamba hii ndo makazi ya wapenzi wa burudani na starehe na hivyo kuwa na fursa kubwa ya programu hii kuonekana kote ulimwenguni.

“Pia ni matumani yangu kuwa uzinduzi wa program hii utavutia watu wengi kutembelea nchi yetu yenye mambo mengi ya kustaajabisha ,” amesema Rais Samia

error: Content is protected !!