
Rais Samia Suluhu Hassan
RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameanza rasmi kurekodi kipindi maarufu cha Royal Tour chenye lengo la kuitangaza Tanzania kimataifa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya kuratibu Mpango wa kuitangaza Tanzania kimataifa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Hassan Abbasi, amesema Rais Samia atatembelea na kuonesha kwa wageni hao vivutio mbalimbali vya utalii, uwekezaji, sanaa na utamaduni vilivyopo nchini.
Rais Samia na wageni hao wa Royal Tour wameanza zoezi hilo la kurekodi maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii na uwekezaji jana Jumamosi, tarehe 28 Agosti, 2021 katika maeneo ya visiwa vya Zanzibar.
Taarifa hii imetolewa leo Jumapili tarehe 29 Agosti 2021 na Jaffar Haniu, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.
More Stories
Chongolo atoa siku 60 kwa MSD kupeleka vifaatiba hospitali Ushetu
NMB yafadhili wiki ya unywaji maziwa Katavi
#LIVE: Tuzo za EJAT2021, Majaliwa atoa ujumbe kwa MCT