Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia aagiza majaji kushughulikia ubora maamuzi mahakama za mwanzo
Habari za Siasa

Rais Samia aagiza majaji kushughulikia ubora maamuzi mahakama za mwanzo

Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan amemuagiza Jaji Mkuu na Kaimu Jaji Kiongozi kutupia jicho vizuri usimamizi wa ubora wa maamuzi kwenye mahakama za mwanzo kwa sababu ndizo zenye malalamiko mengi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Rais Samia ametoa maagizo hayo leo tarehe 6 Oktoba 2021 wakati akizindua jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki katika eneo la National Capital City, Jijini Dodoma.

Uzinduzi rasmi wa jengo hilo lililogharimu Sh bilioni 9 umeenda sambamba na uzinduzi wa majengo matano ya aina hiyo yaliyojengwa katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Morogoro na Dar es Salaam.

“Nawaomba jaji mkuu na kaimu jaji kiongozi, lakini si muda mrefu mtakuwa na jaji kiongozi…. muangalie usimamizi wa ubora wa maamuzi kwenye mahakama za mwanzo. Malalamiko mengi ya mahakama yanahusu mahakama za mwanzo kule kutupiwe jicho vizuri sana,” amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia ameeleza kufurahishwa na jengo hilo lenye huduma za watu wenye mahitaji maalum pamoja na vyumba vya kunyonyeshwa watoto.

“Mahakama tulizo nazo sasa, mama inabidi atafute kichochoro akajifiche, ampe mtoto haki yake halafu arudi mahakamani.”

Pia ametoa wito kwa majaji, mahakimu na watumishi wengine wa mahakama kuongozwa na utashi wa nafsi zai kutoa haki kwa wananchi.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma

“Niwasihi mlipe kipambele kinachostahiki suala la kusikiliza kesi haraka haraka. Msikubali kirahisi kubadilisha mahakimu au kubadilisha tarehe za kusikiliza kesi kwa sababu hilo ndio jambo linalochelewesha kesi,” amesema Rais Samia.

Awali Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Prof Elisante Ole Gabriel amesema Tanzania bara ina upungufu wa watumishi wa mahakama 10,350 kwani waliopo sasa ni 5,835 pekee. Pia kuna upungufu wa mahakama za mwanzo 2996, zilizopo sasa ni 960 wakati zinahitaji 3956.

Hata hivyo, Rais Samia amesema kadiri uwezo wa serikali utakapoendelea kuongezeka ataendelea kuongeza watumishi, kuboresha mazingira ya kazi na pia kuangalia masilahi ya watumishi wa mahakama ikiwa ni pamoja na kukamilisha ujenzi wa makao makuu ya mahakama kuu hapa Dodoma kabla ya Disemba 2022.

Pamoja na mambo mengine amesema ujenzi wa vituo vyote sita umegharimu kiasi cha Sh bilioni 51.5 fedha ambazo ni ni mkopo bilioni 141.9 kutoka Benki ya Dunia ambao serikali imekopa katika maboresho ya mahakama.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Spread the love  NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yaiangukia Serikali kunusuru wananchi Liwale, Nachingwea

Spread the love  CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimeitaka Serikali kuchukua hatua za haraka...

Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani

Spread the love  NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Zungu, watu wanaokwamisha utekelezaji...

Habari za Siasa

Gridi ya Taifa kufumuliwa kukabiliana na katizo la mgao wa umeme

Spread the love  WAZIRI wa Nishati, Januari Makamba, amesema Serikali ina mpango...

error: Content is protected !!