May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Ramaphosa: Uwenyekiti wangu AU kama ubatizo wa moto

Cyril Ramaphosa, Rais wa Afrika Kusini

Spread the love

IKIWA imebaki wiki moja kwa Cyril Ramaphosa, Rais wa Afrika Kusini kuhitimisha mwaka mmoja wa Uenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), amesema kipindi chake kilikuwa kama ubatizo wa moto. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Amesema, nafasi yake ya kusimamia shughuli za umoja huo zimekumbwa na dhoruba kubwa ikiwa ni pamoja na janga la visursi vya corona (COVID-19).

Wiki ijayo, Rais Ramaphosa atamkabidhi kijiti hicho Félix Tshisekedi, Rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambaye naye atasimamia shughuli za AU kwa mwaka mmoja

“Kazi kubwa katika kipindi cha mwaka mzima uliopita ilikuwa ni kuliongoza bara wakati wa kipindi cha janga la dunia la corona.”

“Katika kipindi hicho, eneo huru la biashara (AfCFTA) liliweza kuzinduliwa na kutangazwa kwa ari mpya ya biashara baina ya mataifa ya Afrika na ushirikiano wa kiuchumi,” amesema.

error: Content is protected !!