Thursday , 25 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa BREAKING NEWS: Rais Omar al – Bashir ang’olewa Sudan
KimataifaTangulizi

BREAKING NEWS: Rais Omar al – Bashir ang’olewa Sudan

Spread the love

UTAWALA wa miaka 30 wa Rais wa Sudan, Omar al-Bashir, umefika kikomo nchini humo. Anaripoti Saed Kubenea … (endelea).

Taarifa kutoka mji mkuu wan chi hiyo, Khartoum na miji mingine jirani zinasema, kuangushwa kwa utawala wa al- Bashir, kunatokana na hatua ya jeshi la nchi hiyo, kuagiza kiongozi huyo kung’atuka.

“Jeshi nchini hapa (Sudan), limetangaza kumuondoa madarakani Rais Omar al-Bashir. Mamia ya wanajeshi wametanda katika makazi rasmi ya rais tokea alfajiri ya leo,” anasema mwandishi habari mashuhuri nchini Sudan, Yousra Elbagir.

Anaongeza, “kuna taarifa zinazoeleza pia kuwa baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali, wamekamatwa na jeshi na uwanja wa ndege jijini Khartoum umefungwa.”

Kabla ya hatua hiyo ya jeshi, wananchi walipanga kuendelea na maandamano yao ya kushinikiza rais huyo kuondoka madarakani.

Maandamano dhidi ya al-Bashir yalianza Desemba mwaka jana, ambako wananchi waliingia barabarani kupinga kupanda kwa bei ya vyakula.

Hata hivyo, kadri muda ulivyosogea, ndivyo maandamano hayo yalivyozidi kuwa makubwa na kubadili lengo lake halisi la kupinga ongezeko la chakula na kuelekezwa kwenye “kumng’oa rais Bashir madarakani.”

Taarifa zinasema, magari yaliyosheheni wanajeshi wenye silaha yameegeshwa kwenye barabara zote muhimu na madaraja kwenye mji mkuu, shirika la habari la Reuters linanukuu mashuhuda.

Matangazo ya kawaida ya redio ya serikali yamekatishwa na kwa sasa zinapigwa nyimbo za ukombozi.

Raia wanaimba kwa furaha, “serikali imeangushwa. Tumeshinda,” shirika la Reauters linaripoti.

Maelfu ya watu wamo barabarani wakijaribu kuelekea makao makuu ya wizara ya ulinzi kuungana na waandamanaji ambao wamekuwa wakishinikiza rais Bashir kubwaga manyanga baada ya miaka 30 madarakani. shirika la Habari la kimataifa la AFP linaripoti.

  • Apambana katika jeshi la Misri kwenye vita dhidi ya Israeli mwaka 1973
  • Achukua hatamu ya madaraka Sudan baada ya mapinduzi ya kijeshi mwaka 1989
  • Ampatia hifadhi kiongozi wa al-Qaeda Osama bin Laden katika miaka ya 90.
  • Awa kiongozi wa kwanza wa nchi kufunguliwa mashtaka ICC mwaka 2009.
  • Aingia makubaliano ya amani na waasi wa Sudan Kusini 2005.
  • Akubali Sudan Kusini ijitenge 2011, na kupoteza robo tatu ya utajiri wa mafuta.
  • Hana mtoto, na maisha yake binafsi ni ya usiri mkubwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

error: Content is protected !!