July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Nkurunziza apotea, Tanzania haijui alipo

Waziri wa Nchi za Nje ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akimkaribisha Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza alipokuja Tanzania siku za nyuma

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania inayosimamia mazungumzo ya mgogoro wa kisiasa nchini Burundi imesema haijui alipo Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza ambaye inasemekana serikali yake imepinduliwa.  Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Bernard Membe amewaambia waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuwa: “mimi sijui alipo Nkurunziza”.

Taarifa ya mapinduzi ya serikali ya Burundi ikitangazwa jana, Rais Nkurunziza alikuwa nchini Tanzania kuhudhuria kikao cha Marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kujadili mgogoro wa Burundi. Mpaka sasa hakuna taarifa za uhakikika alipo Rais Nkurunziza.

Baadhi ya vyombo vya habari vya kimataifa zinasema, Nkurunziza aliondoka Tanzania kuelekea nchini kwake, lakini alishindwa kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Bunjumbura, kutokana na uwanja huo kufungwa. 

Habari ambazo hazijathibitishwa zinasema ndege yake ilitua nchini Uganda kujaza mafuta na baadaye kurejea nchini Tanzania.

Akizungumzia kuhusu hali ilivyo nchini Burundi Membe amesema Afrika hawataki tena kuona nchi yoyote, kwa sababu zozote zile, kuchukua madaraka kwa mtutu wa bunduki, badala yake waingia madarakani kwa demokrasia.

“Tukio la jana lililaaniwa na viongozi wote. Lakini zaidi ya hayo baraza la mawaziri wa Afrika Mashariki lililokutana jana na juzi litakutana tena mapema wiki ijayo, kwa ajili ya kufanya tathimini ya hali ya Burundi,” Membe amefafanua.

error: Content is protected !!