Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Rais Nkurunzinza aichomoa Burundi ICC
Kimataifa

Rais Nkurunzinza aichomoa Burundi ICC

Pierre Nkurunziza, Rais wa Burundi
Spread the love

NCHI ya Burundi imekuwa ya kwanza kwa Afrika Mashariki kujiondoa uanachama katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Jinai (ICC).

Serikali ya taifa hilo la Afrika Mashariki ilitoa taarifa ya kusudio lao la kutaka kujindoa ICC kwa Umoja wa Mataifa (UN), kuhusu hatua hiyo mwaka mmmoja uliopita na leo inaweza kuruhusiwa rasmi kujiondoa.

Kulingana na mwandishi wa BBC, Anna Holligan kujiondoa kwa Burundi ni majuto makubwa.

Mahakama ya ICC imeanza kutathmini iwapo inaweza kuchunguza ghasia za kisiasa zilizoibuka baada ya rais Pierre Nkurunziza kuchukuwa madaraka kwa awamu ya tatu, licha ya kuwepo kwa kipindi cha mihula miwili katika katiba ya taifa hilo.

ICC bado ina uwezo wa kuchunguza uhalifu uliotekelezwa wakati Burundi ilipokuwa mwanachama wa mahakama hiyo.

Lakini haiwezi kuchunguza uhalifu wowote wa siku zijazo kwa kuwa haitakuwa tena mwanachama.

Hatua hiyo inaweza kuwa mfano na kuonyesha viongozi wengine kwamba kujiondoa katika mahakama hiyo ni njia mojawapo ya kuepuka jicho la kimataifa hadi pale jamii ya kimataifa itakapochukua hatua na taasisi kama vile Umoja wa

Afrika ama Baraza la Usalama la UN litakapowafuatilia washukiwa na kuyakumbusha mataifa kwamba kujiondoa katika ICC hakumaanishi moja kwa moja kwamba waathiriwa hawatopata haki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!