December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Ndayishimiye: Rais Samia anaibadilisha Tanzania kwa utawala bora

Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye

Spread the love

 

RAIS wa Burundi, Evariste Ndayishimiye, amesema Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, anaendesha nchi kwa kufuata misingi ya utawala bora. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Ndiyashimiye ametoa kauli hiyo leo Ijumaa, tarehe 22 Oktoba 2021, katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika ujenzi w akiwanda cha Mbolea na chokaa cha Itracom, kinachojengwa na muwekezaji kutoka Burundi, jijini Dodoma.

Kiongozi huyo wa Burundi aliyewasili leo nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi, amempongeza Rais Samia akisema anafanya kazi nzuri kuwaunganisha Watanzania na Warundi.

“Napenda kumpongeza Rais Samia kwa kazi anayofanya Tanzania, anaunganisha Watanzania na Warundi, anaendesha nchi vizuri na utawala bora na nchi inabadilika siku kwa siku,” amesema Ndiyashimiye.

Rais Ndayishimiye aliyeingia madarakani baada ya kushinda katika Uchaguzi Mkuu wa Burundi uliofanyika tarehe 20 Mei 2021, yuko nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi ya siku tatu, kuanzia leo hadi tarehe 24 Oktoba mwaka huu.

Kesho Jumamosi, tarehe 23 Oktoba 2021 anatarajiwa kwenda Zanzibar, ambapo atafanya mazungumzo na Rais wa visiwa hivyo, Dk. Hussein Mwinyi, kisha tarehe 24 Oktoba mwaka huu, anatarajia kwenda jijini Dar es Salaam, ambako ataondoka kurejea Burundi.

error: Content is protected !!