Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Mwinyi ‘awaita’ ACT-Wazalendo mezani
Habari za Siasa

Rais Mwinyi ‘awaita’ ACT-Wazalendo mezani

Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar
Spread the love

RAIS wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema, yuko tayari kushirikiana na vyama vingine vya siasa, kuendesha Serikali kama ambavyo Katiba ya Zanzibar inavyoelekeza. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar …(endelea).

Ametoa kauli hiyo leo Jumanne tarehe 11 Novemba 2020 wakati akizindua Baraza la 10 la Wawakilishi Zanzibar.

Dk. Mwinyi ambaye ni Rais wa nane wa Zanzibar, aliingia madarakani tarehe 2 Novemba, 2020 akipokea kiti kilichoachwa na Dk. Ali Mohamed Shein aliyemaliza muhula wake wa miaka kumi ya uongozi.

Rais Mwinyi ametoa pongeza kwa wajumbe wa baraza hilo kwa kuaminiwa na wananchi ikiwemo yeye mwenyewe kwa kuchaguliwa katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 27 na 28 Oktoba 2020.

Katika uchaguzi huo, Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), ilimtangaza Dk. Mwinyi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuibuka na ushindi kwa kupata kura 380,402 sawa na asilimia 76.27 ya kura zote 382,402.

Maalim Seif Sharif Hamad wa ACT-Wazalendo alipata kura 99,103 sawa na asilimia 19.87.

Rais Mwinyi amesema, wananchi “wametuchagua kwa sababu tuna kiu ya kutimiza matarajio yao na heshima yetu itatokana na sisi kutimiza ahadi zetu, maana si tu ahadi bali kutimiza deni ni kulinda heshima.”

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimia na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Zuberi Ali Maulid

“Niwahakikishie, dhamira yangu na  Serikali nitakayoiunda ni kutimiza matakwa ya wananchi wetu,” amesema Rais Mwinyi ambaye ni mtoto wa Rais mstaafu wa Tanzania na Zanzibar, Ali Hassan Mwinyi

Huku akishangiliwa na wajumbe wa baraza hilo, Rais Mwinyi amesema “kura nyingi tulizopigiwa na wananchi ni ishara ya matumaini makubwa ya wananchi kwa chama chetu na kwangu mimi binafsi na ni wajibu wetu sasa kukidhi matarajiuo ya wengi.”

Ametumia fursa hiyo, kuvishukuru vyama vyote vya siasa vilivyoshiriki uchaguzi na kuyapokea matokeo na kuheshimu uamuzi wa wananchi.

“Ninaheshimu maridhiano na matakwa ya Katiba ya kushirikiana na vyama vingimne vya siasa katika kuendesha serikali na niko tayari kuyatekeleza maridhano kama Katiba ya Zanizbar inavyoeleza,” amesema Rais Mwinyi.

Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi

Katiba ya Zanzibar inaelekeza, Serikali ya Umoja wa Kitaifa itaundwa na chama tawala na chama kilichoshika nafasi ya pili ambapo kutakuwa na makamu wawili wa Rais.

Makamu wa kwanza wa Rais, atatokana na chama kilichoshika nafasi ya pili na Makamu wa Pili atatokana na chama kilichoshinda urais.

Pia, Baraza la Mawaziri litahusisha vyama hivyo.

Kwa maana hiyo, katika matokeo ya uchaguzi mkuu, chama ambacho kinakidhi matakwa ya kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni chama cha ACT-Wazalendo.

Hivi karibuni, ACT-Wazalendo wakizungumza na MwanaHALISI Online walisema watakutana kama chama ili kuajdili na kufikia mwafaka wa ama kukubali kushirikiana na Serikali itakayoundwa na Rais Mwinyi au vinginevyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!