July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Mwinyi ateua wakurugenzi wanne, yumo wa ZEC

Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar

Spread the love

 

RAIS wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi, ameteua wakurugenzi wanne, akiwemo Khamis Kona Khamis, aliyemteua kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi visiwani humo (ZEC). Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo Ijumaa, tarehe 16 Julai 2021 na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena Said.

“Rais Mwinyi amefanya uteuzi wa wakurugenzi, Khamis Kona Khamis ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar,” imesema taarifa ya Mhandisi Zena.

Khamis anachukua nafasi ya Thabit Idarous Faina, ambaye ameondolewa katika nafasi hiyo na Rais Mwinyi.

Mbali na uteuzi wa mkurugenzi wa ZEC, Rais Mwinyi amemteua Mohamed Ame Makame, kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar.

Pia, amemteua Said Mtumwa Faki, kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Serikali wa Uchapaji na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali visiwani humo (ZAGPA).

“Bibi Mshauri Khamis Abdulla, ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mipango ya Rasilimali Watu, katika Ofisi ya Rais, Sheria, Utumishi na Utawala Bora. Uteuzi huo unaanzia leo,” imesema taarifa Mhandisi Zena.

error: Content is protected !!