RAIS wa Zanzibar, Hussein Mwinyi amesema, katika hatua anazochukua kuondoa ‘uchafu’ katika Serikali yake, ‘asiyekuwemo hatoingizwa.’ Anaandika Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamao la Jumuiya Tatu za Chama Cha Mapinduzi (CCM), visiwani humo leo Jumatano tarehe 6 Januari 2021, Rais Mwinyi amesema ‘yule atakayekuwemo, atachukuliwa hatua.’
“Kwa hivyo, ombi langu kwenu nyote ni kuunga mkono juhudi za kukabiliana na hali hii,” amesema Rais Mwinyi huku akiungwa mkono na wanakongamano kwa kupiga kelele na vigelegele.
Rais huyo amesisitiza azma yake ya kutofukua makaburi kwa watendaji wabovu waliopita, amesema Watanzania bara na visiwani wameiamini CCM na ndio maana wameipa kura nyingi.
Amesema, hatua zinazochukuliwa na Serikali yake, zinafurahiwa na wengi lakini zinakera wachache huku akisisitiza ‘watuvumilie,’ na kwamba “ili ufanikiwe kulitumbua jibu basi yakupasa kuvumilia maumivu.”
Amewataka viongozi waliochaguliwa kurudi kwa wananchi kutatua shida zao kwa kuwa, baadhi yao huwa na tabia ya kuwasahu wananchi baada ya kuwachagua.
Leave a comment