May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Mwinyi aonya upigaji fedha za Covid-19

Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi

Spread the love

 

RAIS wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi, ameiagiza Wizara ya Afya, ianzishe mfuko maalum wa fedha za vipimo vya ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na Virusi vya Corona (Covid-19), ili kudhibiti upotevu wa fedha hizo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Mwinyi ametoa agizo hilo leo Jumanne, tarehe 6 Julai 2021, katika ziara yake ya kikazi kwenye Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar .

Mwenyekiti huyo wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, amewaonya watu wanaofanya ubadhirifu wa fedha za vipimo vya Covid-19.

“Covid-19 tunawachaji watu kuwapima, tukitengeneza mfuko maalumu wa fedha zinazopatikana na vipimo vya Covid-19. Tukitengeneza mfuko maalumu wa fedha zinazopatikana na vipimo vya Covid-19, “ amesema Rais Mwinyi.

Rais Mwinyi ameongeza; “sina shaka tutapata pesa nyingi zitakazoweza kusaidia ujenzi wa vituo vya afya katika maeneo mbali mbali. Suala hili lisimamiwe vizuri ili kusiwe na ujanja ujanja wa pesa kupotea. Ziwe na mfuko maalumu.”

“Covid-19 tunawachaji watu kuwapima, tukitengeneza mfuko maalumu wa fedha zinazopatikana na vipimo vya Covid-19. tukitengeneza mfuko maalumu wa fedha zinazopatikana na vipimo vya Covid-19, “ amesema Rais Mwinyi.

Rais Mwinyi ameongeza “sina shaka tutapata pesa nyingi tutakazoweza kusaidia ujenzi wa vituo vya afya katika maeneo mbali mbali. Suala hili lisimamiwe vizuri ili kusiwe na ujanja ujanja wa pesa kupotea. Ziwe na mfuko maalumu,.”

Wakati huo huo, Rais Mwinyi ameagiza wizara hiyo kuandaa utaratibu wa kupata fedha za kutekeleza miradi yake ya maendeleo, nje ya bajeti.

“Kwenye upande wa afya nimejionea changamoto zinazokabili sekta ya afya, niseme wizara ya afya bado hatujajipanga sawa sawa. Vituo vya afya havikidhi, sehemu nyingine vipo lakini havitoi huduma na kule huduma zinakotolewa ni duni,” amesema Rais Mwinyi na kuongeza:

“Iko haja ya kuangalia tunafanyaje kuweka uataratibu mzuri, wa kupata hela za kutekeleza huduma za afya kwa maana ya miundombinu ya afya.”

error: Content is protected !!