RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amemkabidhi Afisa mkuu wa Teknolojia na mabadiliko ya kidigitali wa Benki ya NMB, Kwame makundi cheti cha kushukuru udhamini wa NMB kwenye kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Makabidhiano hayo yalifanyika baada ya mchezo wa fainali ya kombe la Mapinduzi Januari 13, 2023 katika uwanja wa Amaani Zanzibar.
Katika mchezo huo uliozikutanisha Mlandege FC ya Zanzibar na Singida Big Star’s ilishuhudia dakika 90 zikimalizika kwa Mlandege kulibakisha kombe hilo baada ya ushindi wa 2-1.
Ni mchezo uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Zanzibar na Tanzanka Bara akiwemo Naibu waziri wa Utamaduni sanaa na michezo, Pauline Gekul.
Pia, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdallah alikuwa miongoni mwa walioshuhudia Mlandege ikirejesha tabasamu kwa Wazanzibar lililokuwa limepotea zaidi ya miaka 10.
Leave a comment