May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Mwinyi ‘afagia’ wahasibu 80 Z’bar

Dk. HUssein Mwinyi, Rais wa Zanzibar

Spread the love

RAIS wa Zanzibar, Hussein Mwinyi amewaondoka kazini zaidi ya wahasibu 80 kwa tuhuma za kuchezea rafu mifumo ya ukusanyaji wa mapato. Anaripoti Mwandishi Wetu. Zanzibar…(endelea).

“Tumewasimamisha zaidi ya wahasibu 80 wa wizara na taasisi zake kwa ajili ya kufanya uchunguzi ambao tumebaini kuchezea mfumo wa ukusanyaji wa mapato ya fedha za serikali,” amesema.

Hatua hiyo amechukuliwa jana Jumatatu tarehe 25 Januari 2021, baada ya Rais Mwinyi kumaliza kuwaapisha makatibu wakuu 15 na manaibu wao saba Ikulu ya Zanzibar ambao waliteuliwa wiki iliyokwisha.

Rais Mwinyi ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi visiwani humo amesema, kumekuwepo na matumizi mabaya ya serikali hasa utoaji wa risiti za mikono.

Kutokana na uchunguzi uliofanywa na watu wake, Rais Mwinyi amewaagiza makatibu wakuu na wasaidizi wao kusimamia ipasavyo maadili ya kazi na fedha za serikali.

“Mchukue hatua maana waziri hata akitaka kufanya lolote anakuagiza wewe, msipofanya hivyo, nitachukua hatua mimi na nitaanzia wizarani,” amesema.

Katika hotuba yake, Rais Mwinyi aliwataka makatibu wakuu hao wapya kutekeleza majumuku yao ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuzisimamia fedha za serikali na kupamabana na uzembe na ufisadi.

Alisema ameamua kupunguza idadi ya manaibu makatibu wakuu kwa lengo la kupunguza ukumbwa wa Serikali pamoja na kupunguza matumizi ya Serikali.

Rais Mwinyi alisema makamtibu wakuu ndiyo maafisa masuuli ambao ndiyo wasimamizi wa fedha za Serikali ambapo aliwataka fedha za mahuduli za Serikali zinapatikana kwani bado kuna taasisi zinakusanya kwa njia ya risiti za mkono na kutaka fedha kukusanywa kwa mtandao.

Aliwataka kuondoa matumizi yasiyokuwa na tija kama vile semina na makongamano pamoja na kuwataka kuondoa aina zote za ubadhilifu, matumizi nje ya bajeti kwani mifumo ya bajeti ya fedha za serikali zimekuwa zikichezewa sana.

error: Content is protected !!