Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Mwinyi aendelea kuteua, kutengua
Habari za Siasa

Rais Mwinyi aendelea kuteua, kutengua

Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar
Spread the love

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameendelea kufanya mabadiliko kwenye serikali kwa kuteua na kutengua viongozi mbalimbali. Anaripoti Victoria Mwakisimba TUDARCo … (endelea)

Dk.Mwinyi aliingia madarakani tarehe 2 Novemba 2020, alipoapishwa kuwa Rais wa nane wa Serikali ya Baraza la Mapinduzi, akichukua kijiti kilichoachwa wazi na Dk. Mohamed Ali Shein, aliyemaliza muda wake wa utawala wa miaka kumi.

Tangu kuingia kwake madarakani, Rais Mwinyi ameendelea kutekeleza kile alichokisema kwamba, atateua na kutengua pale itakapobidi lengo ni kuleta ufanisi katika utendaji kazi.

Leo Jumatano, Rais Mwinyi ameteua wakurugenzi wa sita katika taasisi mbalimbali.

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar, Mhandisi Zena Said amewataja walioteuliwa; ni Dk. Amour Suleiman Mohamed kuwa Mkurugenzi wa Tiba, Dk. Ali Said Nyanga ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya na Dhameera Mohamed Khatib kuwa Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti.

Wengine ni Mwatoum Ramadhan Mussa kuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utendaji, Abdulla Saleh Omar ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Ustawi wa Jamii na Wazee huku Salim Slim Tawakal yeye ameteuliwakuwa Naibu Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya.

Wakati hao wakiteuliwa, jana Jumanne Rais Mwinyi alitangaza kuivunja Bodi ya Ushauri ya Udhibiti wa Vileo Zanzibar ambayo ilikuwa chini ya tawala za mikoa na serikali za mitaa na idara maalum za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Pia, Raisi Mwinyi alitengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Viwango ya Zanzibar (ZBS), Rahima Ali Bakari.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Jaji Biswalo aendelea kung’ang’aniwa fedha za ‘Plea Bargaining’, CUF wataka ajiuzulu

Spread the love  CHAMA cha Wananchi (CUF), kimemtaka aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka...

Habari za Siasa

Bunge labaini madudu mfumo ukusanyaji mapato, h’shauri tatu kikaangoni

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali...

Habari za Siasa

Mkuu wa wilaya ya Rungwe azindua vyumba sita vya madarasa vya thamani ya 64 mil

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu amezindua vyumba...

Habari za Siasa

Mbunge afurahia mabilioni ya Samia kutua jimboni

Spread the love  MBUNGE wa Igunga, Nicholas Ngassa ameishukuru Serikali kwa utekelezaji...

error: Content is protected !!