December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Museveni awataka wasi ADF kujisalimisha

Spread the love

 

RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni aamesema waasi wa kundi Allied Democratic Forces (ADF) linastahili kujisalimisha na kusisitiza kuwa serikali yake imejitolea kukabiliana na ugaidi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Katika hotuba liliyorushwa moja kwa moja kwenye televisheni siku tano baada mashambulio mawili yaliyorindima katika mji mkuu wa Kampala, Museveni alisema ADF wamejiamini kwa sababu wanaweza kutembea huru katika kambi za kijeshi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na wanajishughulisha na uchimbaji madini na biashara za mbao.

Hata hivyo, amesema Uganda itaendelea kuwasaka wanachama wa kundi hilo na kuongeza kuwa ni vyema wale ambao hawajasalimisha silaha zao wafanye hivyo.

Kundi hatari la Islamic State, (IS) lilidai kuhusika na shambulio la Jumanne ambalo lilisababisha vifo vya watu wanne na kuwajeruhi wengine zaidi ya 30.

Aidha, Museveni amesema ADF sasa wamegeukia vitendo vya ugaidi katika maeneo ya mijini baada ya kushindwa katika eneo la Rwenzori na vijijini mwaka 2007.

Tangu mwezi Juni mwaka huu kufuatia jaribio la mauaji ya waziri wa ngazi ya juu yanayoshukiwa kutekelezwa na waasi wa ADF, mashirika ya usalama ya Uganda yamewaua washukiwa 12 na kuwakamata wengine 106.

Miongoni mwa watano kati ya wale waliouawa ni mhubiri wa Kiislamu aliyefariki siku tano zilizopita.

Rais Museveni kwa sasa anafanya mazungumzo mwenzake wa DRC, Rais Felix Tshiekedi kuhusu uwezekano wa kupeleka wanajeshi wa Uganda mashariki mwa Kongo kupambana na kundi la waasi.

ADF ilianza vipi?

Kikundi cha ADF kilianzishwa magharibi mwa Uganda ambapo kiliundwa na wanajeshi waliokuwa wakimuunga mkono Rais wa zamani wa nchi hiyo, Idi Amin na kuanzisha vita vya kupambana na utawala wa rais wa sasa, Yoweri Museveni.

Kikundi hicho kilidai kuwa  utawala huo umekuwa ukiwafanyia maasi.

Kikundi hiki kiliposhindwa na jeshi la Uganda mwaka 2001, kilihamia katika Kivu Kusini katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Baada ya kipindi kirefu cha kusitisha harakati zake, ADF ilisikika tena mwaka 2014 ilipoanza mashambulio ya mara kwa mara dhidi ya raia wa Congo.

Mwaka 2015, ndipo Musa Seka Baluku alipochukua uongozi wa kundi hili baada ya mtangulizi wake Jamil Mukulu kukamatwa. Bakulu alitangaza kujiunga na IS mwaka 2016.

Hata hivyo, kikundi IS kilianza kutangaza kuwa inaendesha harakati zake katika eneo hilo Aprili 2019, ambapo lilikiri kuwa lilitekeleza mashambulio kwenye ngome za kijeshi karibu na mpaka wa Uganda.

IS katika propaganda zake hata hivyo haijawahi kutangaza wazi kuwa IS na ADF waliungana.

Septemba 2020, Baluku alitangaza kuwa kikundi cha ADF hakipo tena.

Alisema, “Sisi kwa sasa tuko jimbo la Afrika ya kati, mojawapo ya maeneo yanayounda Islamic State.”

error: Content is protected !!