Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Makala & Uchambuzi Rais mtata wa Ufilipino, Rodrigo Duterte, tangaza kujiuzulu siasa
Makala & Uchambuzi

Rais mtata wa Ufilipino, Rodrigo Duterte, tangaza kujiuzulu siasa

Spread the love

RAIS wa Ufilipino, Rodrigo Duterte amesema, tofauti na ambavyo alieleza huko nyuma, ameamua kujiuzulu siasa na hivyo, hatajitosa katika kinyang’anyiro cha urais katika uchaguzi mkuu ujao. Anaripoti Matilda Buguye…(endelea).

Duterte mwenye umri wa miaka 76, alieleza Septemba mwaka huu, kwamba hatagombea kiti cha makamu wa rais mwaka 2022. Katiba ya Ufilipino imeweka kikomo cha muhula mmoja wa miaka sita kwa kila rais.

Amesema, ameamua kujiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho kwa kuwa “hisia za Wafilipino wengi, ni kwamba sifai kuwa kiongozi wao.”

Haya yanaibuka wakati huu, ambako kumeibuka uvumi kwamba binti yake, Sara Duterte-Carpio, anaweza kugombea nafasi inayoshikiliwa na baba yake.

Kwa sasa, Sara ni meya wa Davao, mji uliyopo kusini mwa nchi hiyo.

Bw. Duterte, mtu mwenye utata, aliingia madarakani mwaka 2016, ambapo aliahidi kupunguza uhalifu na kutatua mzozo wa madawa ya kulevya nchini mwake.

Hata hivyo, wakosoaji wake wanasema, katika kipindi cha miaka mitano cha uongozi wake, Duterte amechochea polisi kufanya mauaji na ukiukaji wa sheria kwa washukiwa katika kile alichokiita, “vita dhidi ya mihadarati.”

Mwezi uliyopita, Sara alinukuliwa akisema, hatajitosa kwenye kinyang’anyiro cha urais, kwa sababu yeye na baba yake, wamekubaliana kuwa ni mmoja kati yao tu, ndiye atakayegombea katika uchaguzi wa Mei mwakani.

Hata hivyo, aliongoza katika kura za maoni zilizofanyika mwaka huu.

Tangazao la ghafla la kujiuzulu amelitoa mjini Manila, eneo ambalo alikuwa anatarajiwa kujisajiri kama mgombea, na kuongeza, “kugombea kama makamu wa rais, ni kukiuka katiba.”

Ingawa Harry Roque, msemaji wa Duterte hakueleza ikiwa kiongozi huyo ataondoka kabisa kwenye ulingo wa kisiasa, lakini amesema, tangazo hilo “linamaanisha kuwa hana haja na kuwa makamu wa rais.”

Ameongeza, “kuhusu iwapo atajiuzulu kabisa na kutoka katika siasa, nitahitaji kupata thibitisho la hili kutoka kwake.”

Hata hivyo, wachambuzi wa mambo wanasema, tangazo la Duterte linapaswa kuchukuliwa kwa umakini. Ana mtindo wa kusema mambo yanayofanana na hayo, na baadaye kugeuza usemi wiki moja baadaye.

Kwa mfano, Septemba mwaka 2015, wakati wa kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu, akiwa meya wa Davao wakati huo, Duterte alisema, alikuwa amepanga kujiuzulu maisha ya umma daima.

Lakini katika hatua ya dakika za mwisho, Novemba mwaka jana, Duterte alichaguliwa kama mgombea wa chama cha PDP-Laban na kushinda urais, Mei 2016.

Wakati alipotangaza kwa mara ya kwanza nia yake ya kugombea, kulikuwa na tetesi kuwa atamchagua mgombea mwenza dhaifu kisiasa ili aweze kuendelea kuongoza akiwa makamu wa rais.

Alishawahi kusema hilo hadharani, kwamba kama makamu wa rais, atakuwa na kinga dhdi ya kushitakiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), kufuatia madai ya kuongoza ukatili wa “vita kuhusu mihadarati” ambavyo viliwauwa maelfu ya watu nchini Ufilipino.

Haijafahamika sasa, kwamba kuamua kwake kutohombea nafasi hiyo, kutamuondolea kinga hiyo hiyo ya kisheria.

Kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binadamu la kimataifa Amnesty International, zaidi ya watu 7,000 (elfu saba), waliuliwa na polisi au washambuliaji wasiojulikana katika miezi sita ya kwanza ya urais wake.

Juni mwaka huu, mwendesha mashitaka wa ICC aliomba kufungua uchunguzi kamili kuhusu mauaji ya vita vya mihadarati katika Ufilipino, akisema kuwa uhalifu dhidi ya binadamu huenda ulifanyika.

Waandishi wa habari wanasema, iwapo Bi Duterte-Carpio atachaguliwa kuwa rais, kutakuwa na uwezekano mkubwa wa kumlinda baba yake dhidi ya mashitaka ya uhalifu ndani ya Ufilipino na mashitaka ya ICC.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaMakala & Uchambuzi

Kanda ya Ziwa yaonyesha NMB inavyosaidia afya ya mama na mtoto

Spread the loveMafanikio inayozidi kupata Tanzania katika kupunguza vifo vya mama na...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

‘Mwanapekee’ wa Rais Samia: Atabadili nini Arusha?

Spread the loveMAPEMA wiki hii, baadhi ya viongozi walioapishwa na Rais Samia...

Habari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kipunguni waihoji serikali, ziko wapi fedha za fidia?

Spread the loveWATU wanaodai kwamba serikali ya Chama Cha Mapinduzi ni sikivu,...

Habari za SiasaMakala & UchambuziTangulizi

Askofu Bagonza: Tusichonganishwe; tusichokozane na tusikufuru

Spread the loveJOTO la chaguzi linapanda kila siku hapa nchini. Upo umuhimu...

error: Content is protected !!