May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Msumbiji awatimua waziri ulinzi, mambo ya ndani

Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi

Spread the love

 

RAIS wa Msumbiji, Filipe Nyusi amemfuta kazi Waziri wa ulinzi wa nchi hiyo, Jaime Augusto Neto bila kufafanua sababu halisi za kumchukua uamuzi huo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya rais kumfukuza kazi Waziri wa mambo ya ndani, Amade Miquidade.

Taarifa iliyotolewa jana tarehe 10 Novemba, 2021 na Ofisi ya Rais Ikulu, imeseme Rais amemfuta kazi waziri huyo bila kueleza kwanini amewafuta kazi viongozi wakuu wa ulinzi na usalama wa nchi.

Aidha, inaelezwa kuwa uamuzi huo unahusiana na kuongezeka kwa visa vya utekaji nyara, mauaji, ugaidi na ufisadi, pamoja na kuongezeka kwa idadi ya ajali za barabarani.

Baadhi ya kesi hizo zimehusisha askari wa ulinzi na usalama.

Waangalizi wa mambo ya usalama wamemtaka Rais Nyusi kueleza maamuzi yake ili kuepuka uvumi, hofu na kuibua fujo.

Wanasema si jambo la kawaida kuwatimua viongozi wawili wakuu wa usalama kwa siku chache na kwamba lazima kuwe na sababu.

error: Content is protected !!