RAIS wa zamani wa Algeria, Abdelaziz Bouteflika aliyefariki dunia siku ya juzi, anatarajiwa kuzikwa leo tarehe 19 Septemba 2021 katika makamburi ya mashujaa ya El Alia jijini Algiers nchini humo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Licha ya kuzikwa katika makaburi hayo yaliyotengwa kwa ajili ya mashujaa wa vita vya uhuru, Rais huyo hatazikwa kwa heshima zote sawa na watangulizi wake.
Bouteflika aliyeondolewa madarakani mwaka 2019 baada ya kuitawala Algeria kwa miaka 20, alifariki dunia tarehe 17 Septemba akiwa na umri wa miaka 84 katika nyumba yake huko Zeralda (Magharibi mwa Algiers) alikoishi alikuwa akiishi kwa miaka miwili na nusu.
Kwa mujibu wa televisheni ya taifa hilo, atazikwa baada ya sala ya Dhuhur sawa na saa sita mchana sa za kimataifa.

Mwili wake utapelekwa makao makuu ya Bunge, katikati mwa Algiers ambapo viongozi mbalimbali serikalini na raia watatoa heshima za mwisho, kabla ya kuelekea kwenye makaburi ya El Alia, umbali wa kilomita 10.
Katika uwanja huo mashujaa, makaburi ya watangulizi wake wote walizikwa, ikiwa ni pamoja na watu mashuhuri na mashujaa wa vita vya uhuru (1954-1962).
Algeria imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kuanzia jana tarehe 18 Septemba 2021, kufuatia kifo cha rais huyo wa zamani.
Ofisi ya rais huyo wa sasa ilisema katika maombolezo hayo ya siku 3 bendera zitapepea kwa nusu mlingoti.
Leave a comment