May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Mseven afunga shule, baa na makanisa Uganda

Spread the love

 

RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni, ametangaza kufungwa kwa shule na taasisi za elimu ya juu na kusitisha mikusanyiko ya watu nchini humo kwa siku 42, kuanzia leo Jumatatu, tarehe 7 Juni 2021. Inaripoti Mitandao ya kimataifa … (endelea).

Ni baada ya nchi hiyo kukabiliwa na maambukizi mengi katika wimbi la pili la la ugonjwa wa corona (Covid-19).

Pia, baa na kumbi za sinema zimefungwa.

Tangazo hilo ni saa kadhaa baada ya wizara ya afya nchini humo, kutangaza maambukizi mapya 1,259 ya corona ambapo ni idadi kubwa zaidi ya maambukizo yaliyorekodiwa jana Jumapili, kwa siku moja na vifo tisa.

Amesema, usafiri wa umma nao utapigwa marufuku kuanzia Alhamisi ili kupisha wanafunzi ambao wako shuleni warudi nyumbani.

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni

Museveni amesema, walimu wote watapaswa kupewa chanjo kabla ya shule na vyuo kufunguliwa.

“Kuna ongezeko kubwa la maambukizi mashuleni tangu Mwezi Machi, wagonjwa 948 wameripotiwa kwenye shule 43 kutoka wilaya 22, naamini namba hii ni kubwa zaidi , shule zingine hazitoi takwimu kwa kuwa hawataki zifungwe na wengi wanawaza pesa tu” amesema Rais Museveni.

Hospitali ya rufaa ya Taifa ya Mulago, iliripoti kuongezeka kwa wagonjwa wa Covid-19 wiki iliyopita, ikisema inahitaji kuongeza vikitanda kwa ajili ya wagonjwa. hadi sasa, Uganda ina maambukizi 52,929 vya corona na vifo 374.

error: Content is protected !!