January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais mpya wa Zambia aanguka akihutubia wanawake

Rais wa Zambia, Edgar Lungu

Spread the love

MIEZI miwili tangu achaguliwe kuongoza Zambia, kuchukua nafasi ya mtangulizi wake Michael Sata, aliyefariki kwa ugonjwa, Rais mpya wa nchi hiyo, Edgar Lungu, amezua hofu kwa wananchi baada ya kuanguka jukwaani.

Lungu ambaye amechaguliwa Januari mwaka huu, alianguka wakati akisoma hotuba yake katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, yalifanyika mji mkuu wa Lusaka.

Kwa mujibu wa daktari wake, Lungu alitarajiwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya upasuaji wa koo, na baadaye ilithibitika kwamba pia anasumbuliwa na ugonjwa wa malaria.

Wakati wa kampeni, washirika wa Lungu walikanusha ripoti kwamba alikuwa mgonjwa na kuwa alishauriwa kwenda nje ya nchi kwa uchunguzi wa afya yake.

Uchaguzi wa Zambia uliomleta Lungu madarakani, uliitishwa kufuatia kifo cha mtangulizi wake, Michael Sata ambaye naye alikuwa amechukua nafasi hiyo baada ya kifo cha Rais Levy Mwanawasa.

Lungu (58), alitibiwa katika hospitali ya mjini humo na ofisi yake imetoa ripoti ya kuwahakikishia Wazambia kwamba rais wao “unaendelea vizuri” na kwamba atarudi nchini Jumatatu, pasipo kutaja anatibiwa wapi.

Taarifa kutoka ofisi ya rais imesema Lungu alikuwa anasumbuliwa na “esophagus” nyembamba ambazo zinahitaji utaratibu wa utaalamu wa hali ya juu wa teknolojia ya matibabu ambayo sasa hayapo katika Zambia.

error: Content is protected !!