April 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Moi afariki dunia

Daniel arap Moi, Aliyekuwa Rais wa Kenya (1978-2002).

Spread the love

RAIS wa Pili wa Kenya, Daniel arap Moi (95), amefariki dunia usiku wa kuamkia leo tarehe 4 Februari 2020. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Uhuru Kenyatta, rais wa sasa wa taifa hilo, ametangaza msiba huo jana usiku. Taarifa zaidi kutoka nchini humo zinaeleza, Rais Moi alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Nairobi.

Rais huyo mstaafu, alianza kushika madaraka makubwa mwishoni mwa mwaka 1964, baada ya Rais Jomo Kenyatta kuwa Rais wa Kwenya ambayo yeye aliteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani.

Mwaka 1967 Rais Moi alimteuwa kuwa Makamu wa Rais pia Naibu Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge wa Kanu. Kenyatta alipokuwa Agosti 1978, Rais Moi aliteuliwa kaimu nafasi ya urais wa Kenya.

Uchaguzi Mkuu ulipofanyika Oktoba 1978, Rais Moi alichaguliwa kuwa Rais wa Kenya. Alinusurika kupinduliwa mwaka 1982 baada ya wanajeshi wanaomtii kukabili mapinduzi hayo.

error: Content is protected !!