April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Moi aagwa kwa aina yake bungeni

Daniel arap Moi, Aliyekuwa Rais wa Kenya (1978-2002).

Spread the love

MAELFU ya raia na viongozi wa Serikali ya Kenya, leo tarehe 8 Februari 2020, wamejitokeza katika viwanja vya bunge jijini Nairobi, kutoa heshima za mwisho kwa Daniel Arap Moi, Rais Mstaafu wa Nchi hiyo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Katika hali isiyo ya kawaida, wananchi hao walitoa heshima zao za mwisho kwa Rais Moi, ambaye mwili wake  uliwekwa juu ya meza, badala ya kuwa ndani ya jeneza.

Zoezi hilo liliongozwa na Rais Uhuru Kenyatta, ambapo baada ya hapo mwili wa rais huyo mstaafu wa Kenya, utatembeza katika viunga vya barabara za Jiji la Nairobi, kwa ajili ya kutoa fursa kwa wananchi kutoa heshima zao za mwisho.

Mamlaka nchini Kenya zimefunga barabara za jiji la Nairobi kwa muda wa siku tatu kwa ajili ya kupisha zoezi hilo. Huku bendera zikipeperushwa kw anusu mlingoti hadi mwili wa marehemu utakapizikwa.

Mwili wa Rais Moi unatarajiwa kuagwa kwa mara ya mwisho pamoja na kufanyiwa ibada katika Shule ya Msingi Kabarak, kisha utazikwa siku ya Jumatano ya tarehe 12 Februari 2020, nyumbani kwake Kabark, Nakuru nchini humo.

Rais Moi alifariki dunia tarehe 4 Februari mwaka huu, katika Hospitali ya Nairobi, alikolazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

error: Content is protected !!