September 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwili wa Rais Mkapa kuagwa Uwanja wa Taifa

Spread the love

MWILI wa Benjamin Mkapa, Rais wa Awamu ya Tatu ataagwa katika Uwanja wa Mpira wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa na Kasim Majaliwa, Waziri Mkuu wakati akizungumza na watu waliofika nyumbani kwa Hayati Mkapa, Masaki, jijini Dar es Salaam leo tarehe 24 Julai 2020.

“Kamati ya mazishi ya serikali inaandaa taratibu zote baada ya kupata taarifa ya familia, tutatoa taarifa ya kitaifa siku ya maombolezo ya kitaifa ambapo awali yatafanyika hapa Dar es Salaam, Uwanja wa Taifa,” amesema Waziri Majaliwa.

Hata hivyo, kwenye taarifa hiyo Waziri Majaliwa hajasema siku wala tarehe ambayo shughuli hiyo ya kuaga mwili wa Mkapa itafanyika.

Saa sita usiku wa kuamkia leo, Rais John Magufuli aliutangazia umma kifo cha Rais Mkapa kilichotokea hospitali alikokuwa amelazwa jijini Dar es Salaam.

Kwenye ukurasa wake wa twitter Rais Magufuli ameandika:- “Nimesikitishwa na kifo cha Mzee wetu Benjamin Mkapa (Rais Mstaafu wa Awamu ya 3). Nitamkumbuka kwa mapenzi yake makubwa kwa Taifa, ucha Mungu, uchapakazi na utendaji wake katika kujenga uchumi. Hakika Taifa limepoteza nguzo imara. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina.”

error: Content is protected !!