April 15, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Mkapa ateuliwa tena kuwa Mkuu wa UDOM

Chuo Kikuu cha Dodoma

Spread the love

RAIS John Magufuli amemteua Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Anaripoti Regina Mkonde … (endelea). 

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo tarehe 14 Mei 2019 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Gerson Msigwa.

Taarifa ya Msigwa inaeleza kuwa, Rais Magufuli amemtea Mkapa kushika wadhifa huo kwa kipindi cha pili mfululizo.

Aidha, Rais Magufuli amemteua Profesa Ignas Rubaratuka kushika wadhifa wa Uwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) kwa kipindi cha pili mfululizo.

“Uteuzi wa viongozi ho umeanza tarehe 10 Mei 2019,” inaeleza sehemu ya taarifa ya Msigwa.

error: Content is protected !!