December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Marekani, Kenyatta wateta Ikulu, chanjo ya corona milioni 17 kutolewa Afrika

Spread the love

 

RAIS wa Marekani, Joe Biden amekutana na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta Ikulu ya White House huku Biden akiahidi kutoa dozi milioni 17 ya chanjo ya corona. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mazungumzo hayo yaliyofanyika jana Alhamisi, tarehe 14 Oktoba 2021, Ikulu ya White House, Marekani huku Kenyatta akiwa Rais wa kwanza wa kutoka Afrika kuteta Ikulu na Biden.

Rais Biden amemshukuru Kenyatta kwa kukubali mwaliko wake na kuahidi kushirikiana baina ya mataifa hayo mawili ikiwemo kukuza amani na masuala ya ulinzi na usalama.

Ninafurahi kuwa na Rais wa Kenya hapa, Rais Kenyatta. Ninashukuru kukukaribisha White House, karibu sana,” amesema Rais Biden huku Kenyatta akiitikia “nashukuru sana Rais. Nisema nafurahi kuonana nawe tena.”

Kuhusu mapambano ya maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19), Rais Biden ameahidi kutoa chanjo ya corona dozi milioni 17 aina ya Johnson & Johnson kwa nchi za Umoja wa Afrika (AU).

“Tutaendelea kushirikiana katika mapambano ya COVID-19. Marekani imekwisha kutoa dozi milioni 2.8 kwa Kenya kati ya dozi milioni 50 na tutatoa dozi kwa Umoja wa Afrika (AU),” amesema Rais Biden, aliyeingia madarakani Januari 2021 baada ya kumshinda Donald Trump

Kwa upande wake, Rais Kenyatta amemshukuru Biden kwa kumpa fursa ya kuteta naye na kuahidi kushirikiana na Marekani katika mapambano dhidi ya ugaidi unaoikabili dunia.

Aidha, Rais Kenyatta amesema, eneo jingine ni kushirikiana katika mapambano ya mabadiliko ya tabia ya nchi.

error: Content is protected !!