March 7, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli: Waliozamisha MV Nyerere wakamatwe, maombelezo siku nne

Rais John Magufuli

Spread the love

SERIKALI imeagiza vyombo vya dola kuwakamata na kuwahoji wahusika katika uendeshaji safari za kivuko cha MV Nyerere kuhusu ajali ya kivuko hicho iliyotokea jana tarehe 20 Septemba 2018. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Vilevile, Rais John Magufuli wakati akizungumzia kuhusiana na ajali hiyo ametangaza siku nne za maombolezo kuanzia leo tarehe 21 hadi 24 Septemba 2018. Kwa kupeperusha Bendera zote za serikali nchini nusu mringoti kwa siku tatu kuanzia kesho.

Akitoa taarifa rasmi ya serikali kuhusu ajali hiyo leo tarehe 21 Septemba 2018, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi amesema baada ya wahusika hao kuhojiwa na kubainika kufanya uzembe uliosababisha ajali hiyo, watachukuliwa hatua za kisheria.

“Lakini katika hatua nyingine serikali imeagiza wahusika wote katika uendeshaji safari za kivuko hichi wakamatwe na wahojiwe, kila ambaye alikuwa nahusika na operesheni za kivuko hiki watakamatwa na kuhojiwa maelezo yake ili kujua ushiriki wa kila mmoja katika janga hili ulikuwa ni upi? Na kwa wale watakaobainika kwamba ni washiriki wa moja kwa moja basi watachukuliwa sheria kwa mujibu wa sheria,” amesema Balozi Kijazi.

Katika hatua nyingine, Balozi Kijazi amesema uchunguzi wa awali umebainisha kuwa, chanzo cha ajali hiyo ni kivuko kubeba abiria wengi kuliko uwezo wake.

DnitYLXWwAEDLUS

 “Uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba chanzo cha ajali hiyo ni kubeba abiria zaidi ya uwezo wake, kivuko hicho kinatakiwa kubeba abiria 101, kwa hiyo unaweza kupiga mahesabu 40 waliokolewa wakiwa hai, 127 wamefariki jumla ni 167 tayari 66 wamezidi, na hatujui ni abiria wangapi wengine miili yao iko majini.

“Serikali ianendelea na uchunguzi wa kina ili kujithibitishia kwa uhakika ili kujua ajali hiyo imetokana na sababu zipi, baada ya uchunguzi huo tutatoa taarifa kwa wananchi kwamba chanzo ni nini,” amesema.

Balozi Kijazi amesema hadi kufikia leo saa tisa na dakika 10 mchana abiria waliokuwa kwenye kivuko hicho ambao wameokolewa wakiwa hai walikuwa ni 40, na waliopoteza maisha ni 167.

error: Content is protected !!