January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli umesikia hospitali ya Mwanza

Spread the love

HOSPITALI ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure, inakabiliwa na changamoto ya vifaa pamoja na mtaalamu wa tiba ya mfupa kitendo kinachosababisha wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kukosa huduma. Anaandika Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Hayo yamesemwa jana na Afisa Ustawi wa Jamii, Leah Linti, kwa niaba ya Katibu wa Hospitali hiyo, Danny Tembo, wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya changamoto zinazoikabili hospitali hiyo.

Amesema licha ya hospitali hiyo kupokea wagongwa mbalimbali wakiwamo waliovunjika mfupa, wanakabiliwa na tatizo la mtaalamu wa mfupa kitendo ambacho kinawalazimu wagonjwa kupeleka katika Hospitali ya Rufaa Bugando (BMC).

Linti amesema licha ya hospitali hiyo kuwa na mahitaji ya vifaa kama vile Ecco na CT Scan lakini bado dalili za upatikanaji wa vifaa hivyo bado ni kitendawili jambo linalohitaji jitihada za haraka.

“Hapa sisi vifaa ambavyo tunavyo ni vya X-ray, Ultra Sound na vingine vya maabara, kama mgonjwa aliyevunjika mfano mkono hatuwezi kumtibu, tunaomba serikali iliongia madarakani kuangalia suala hili.

“Sekou Toure tunapokea wagonjwa 300 hadi 400 kwa siku, watalaamu walipo ni 400 na ili tukabiliane na wingi huu tunapaswa kuwa nao 600 na zaidi,” amesema Linti.

Hata hivyo Linti alimuomba Rais John Magufuli, kuhakikisha anaboresha hospitali za wilaya ambazo alidai kutokana na ukosefu wa dawa na vifaa, zinachangia idadi kubwa ya wagonjwa hospitalini hapo.

Muuguzi Mkunga katika wodi ya wazazi, Veronica Ngowi, amesema kwenye wodi hiyo kwa siku hupokea wakina mama 55 – 60 wanaojifungua kitendo kinachochangia kutolewa kwa huduma.

“Hii wodi wagonjwa tunaopokea ni wengi na vitanda vilivyopo ni 73, hivyo sasa tatizo la kulala watatu kwenye kitanda kimoja haliepukiki, naomba serikali kuangalia hali hii,” amesema Ngowi.

error: Content is protected !!