October 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli: Uchaguzi Mkuu palepale

John Magufuli, Rais wa Tanzania

Spread the love

LICHA ya kuwepo kwa tishio la kusambaa kwa virusi vya corona (COVID-19) nchini, uchaguzi mkuu unaoratajiwa kuwanyika Oktoba mwaka huu, hautaahirishwa. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Akizungumza jijini Dodoma leo tarehe 26 Machi 2020, Rais John Magufuli amesema, uchaguzi huo hautasogweza mbele, kwa kuwa hakuna mtu anayetaka kuendelea kukaa madarakani.

Ametoa kauli hiyo huku kukiwa na taarifa zisizothibitishwa kwamba, uchaguzi huo utafanyika mwaka 2021 kutokana na tishio la ugonjwa corona.

“Hatujazuiliwa kukutana, sisi tunaendelea kukutana na tunakutana katika mikutano ya kawaida, na uchaguzi tutafanya tu, wako wengine wanafikiri nitaahirisha, nani anataka kukaa kwenye maofisi muda wote huo?” amehoji Rais Magufuli.

Rais Magufuli amesema, kazi zitaendelea kufanyika ikiwemo vikao vya bunge vitaendelea.

“Hatujazuiliwa kukutana, leo nilikuwa nasoma gazeti moja linasema Madiwani wafanya kikao sijui alifikiri wamezuiliwa kukutana kwa sababu ya Corona? Sisi tunaendelea kukutana, hata nchi zilizoathirika, bado mabunge na mabaraza hayajafungwa,”amesema Rais Magufuli.

error: Content is protected !!