Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli: Tumefanikiwa
Habari za Siasa

Rais Magufuli: Tumefanikiwa

Rais wa Tanzania, John Magufuli
Spread the love

TANZANIA imetajwa kuwa nchi ya kwanza kwa utulivu na amani katika Ukanda wa Afrika Mashariki, pia imeshika nafasi ya saba katika nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kauli hiyo ameitoa leo tarehe 16 Juni 2020, jijini Dodoma wakati akifunga Bunge la 11 kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kutoa fursa mchakato wa uchaguzi mkuu kuanza.

Amesema, wakati akiingia madarakani kulikuwa na wimbi kubwa la uhalifu wa kutumia silaha na mauaji jambo ambalo vikosi vya ulinzi na usalama limesimamia na kumaliza matukio hayo.

“Ripoti ya Global Peace Index 2020 imeitaja Tanzania kushika nafasi ya kwanza kwa amani na utulivu kwenye eneo la Afrika Mashariki, na nafasi ya saba kwa nchi zilizoko Kusini mwa Jangwa la Sahara, kwa niaba ya Watanzania wote navipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kazi kubwa.

“Wakati tukiingia madarakani, kulikuwa na wimbi kubwa la uhalifu wa kutumia silaha, pamoja na matukio ya mauaji kule Kibiti na kupitia Vyombo vya Ulinzi na Usalama vitendo hivyo vilikomeshwa na nipende kusema kuwa nchi yetu kwa sasa ni salama,” amesema Rais Magufuli.

Amesema, wakati akiingia madarakani, miongoni mwa ahadi yake katika utawala wake ni kudumisha amani na mshikamano ambavyo sasa vimeshuhudiwa nchini.

“Mojawapo ya ahadi kubwa niliyoitoa wakati wa kuzindua Bunge ni kudumisha amani, umoja, mshikamano, ninayo furaha kuwa tumetimiza ahadi hiyo kwa vitendo kwani Watanzania tumeeendelea kuwa wamoja na kushirikiana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

Habari za SiasaTangulizi

Maafa Manyara: Rais Samia akatisha ziara yake Dubai

Spread the loveRAIS wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amekatisha ziara yake...

Habari za SiasaTangulizi

Wataalaam wa miamba watua Hanang

Spread the loveWaziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na...

error: Content is protected !!