August 16, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli: Nitawanyoosha

Spread the love

RAIS John Magufuli ameapa kuwanyoosha wale wanaotafuna fedha za wananchi badala ya kuzielekeza katika maendeleo, anaandika Regina Mkonde.

Pia ameeleza furaha yake baada ya Bunge la Jamhuri kupitisha sheria ya kuwabana mafisadi akidai kuwa, sasa atawanyoosha.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo wakati akihutubia katika uzinduzi wa Mpango wa Usalama wa Jamii uliofanyika katika viwanja vya Biafra, jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa, ni lazima serikali iende mbele kwa yale iliyoyaahidi sambamba na kushukuru kupitisha muswada wa kushughulikia mafisadi.

“Ninapenda kulishukuru sana Bunge kwa kupitisha muswada huo wa kushughulikia mafisadi, ili mafisadi wanyooke kweli kweli.

“Tanzania tunahela nyingi lakini watu wanakula kweli kweli lakini hawashibi, ila tufikie mahali tuwalazimeshe washibe kwa nguvu kwa hizi hatua tutakazochukua,” amesema.

Pia ameagiza Taasisi ya ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kufanya uchunguzi wa mkataba wa ujenzi wa barabara zilizopo katika Manispaa ya Kinondoni zinazoonekana kujenjwa chini ya kiwango.

“…pamoja na injinia aliyesimamia huo mradi, ninafahamu aliyekuwa injia wa jiji hili nafikiri ni Kinondoni tulisimamisha kazi, na vyombo vya PCCB vianze kuchunguza.

“Hivi ni vitu vya kuweza kushughulikiwa, wananchi wamechoka fedha zao kuwa zinatumiwa na watu wachache, ifike mahali watu waliokuwa na mazoea ya kula mali za umma waanze kuogopa wakale mali za bibi zao kule,”amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amteoa agizo hilo baada ya Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kushitaki kwamba, wananchi wa mkoa huo wamechoka kujengewa barabara zisizo za viwango.

“Wananchi wamechoka kujengewa barabara zilizochini ya kiwango, imekuwa kilio cha muda mrefu, pesa nyingi zinatumika kujengea barabara na matokeo yake barabara zinakuwa mbovu na kila mwaka zinajengwa barabara zile zile wakati wananchi wanatamani barabara zenye viwango vya rami,” amesema na kuongez;

“Nikiwambia tu hapa mbele yako ipo barabara iliyojengwa na haijamaliza hata mwaka mmoja ambayo inatokea Ubalozi wa Ufaransa inakuja hapa tulipo Biafra inaenda mpaka Mwanaymala, hii ingesaidia kupunguza foleni imeishaanza kuharibika na ni mbovu.”

Makonda amesema, mkataba uliokuwepo kwenye Manispaa ya Kinondoni unaeleza kuwa, ilitakiwa mkandarasi alipwe Sh. 500 milioni na kwamba, aliongezewa Sh. 400 milioni kinyume na taratibu pia alijenga barabara chini ya kiwango.

“Na ajabu kwa mkataba huu uliopo wa Manispaa ya Kinondoni ambapo walimlipa milioni 500 na kuongezewa milioni 400.

“Nimemuagiza mkurugenzi na mkuu wa wilaya kuhakikisha anajenga barabara kwa gharama zake na zile pesa zilizotolewa kinyume na taratibu zirudishwe.

“Jana mimi na wakuu wa wilaya tuliamua kusitisha kampuni nne zisipewe leseni katika mkoa wetu mpaka watakapothibitisha wana uwezo wa kujenga barabara zenye ubora,” amesema.

Amesema, mkandarasi yeyote atakayejenga barabara isiyo na kiwango kwenye Mkoa wa Dar es Salaam, hatapata tenda tena.

error: Content is protected !!