May 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli: Nimemsamehe Andengenye lakini… 

Thobias Andengenye, aliyekuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Magufuli ametangaza hadharani kumsamehe aliyekuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye ambaye alimuomba msamaha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Amesema, licha ya kumsamehe Andengenye lakini hatomrudisha ndani ya jeshi hilo na atamtafutia kazi eneo jingine.

Rais Magufuli ametoa msahama huo leo Alhamisi tarehe 11 Juni 2020 wakati akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa jengo la ofisi ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji jijini Dodoma.

Amesema amefikia hatua hiyo baada ya Andengeye kumuomba radhi mara kadhaa, kufuatia.

“Mliopo hapa mkafikishie salamu kwamba nimemsamehe na hapa kwa sababu ameomba msamaha zaidi ya mara tatu, ni unyenyekevu wa aina yake, lakini kwenye jeshi hili hatarudi mtamuona katika maeneo mengine,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufulii amesema viongozi waliopo sasa katika jeshi hilo wameufanyia marekebisho mkataba uliomfanya kumwondoa kwenye nafasi hiyo Andengenye.

Aidha, Rais Magufuli amewataka maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kuwa waaminifu na fedha za umma, kwa kuwa katika uongozi wake hakuna fedha za bure.

“Niwaombe sana ndugu zangu wa zimamoto yaliyopita si ndwele tuyasahau na tusiyarudie. Fedha za bure katika kipindi changu ni mbaya zitawaharibia katika maisha yenu na mimi hata mloge namna gani sibadiliki,” amesema

Pia, Rais Magufuli ametoa msahama kwa makamishna wengine wa jeshi hilo ambao alipelekewa mapendekezo ya kuwashusha vyeo na kuwaondoa ndani ya jeshi hilo akisema, “nafahamu kulikuwa na mapendekezo ya makamishina kama wanne kuwateremsha cheo na wengine kuwafukuza, nimeangalia mnavyopendeza, mlivyo na huruma na nyuso zenu zinaonesha mmetubu, nimewasamehe.”

Msamaha huo unatokana na RAIS Magufuli kumwondoa katika wadhifa wa Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo  kufuatia sakata la mkataba tata wa ununuzi wa vifaa vya uoakoaji, wenye thamani ya zaidi ya Sh. 1 trilioni.

Kamishna Andengenye alifutwa kazi na Rais Magufuli tarehe 23 Januari 2020 katika hafla ya ufunguzi wa nyumba za askari Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam.

Pamoja na Andengenye, mwingine aliyeng’oka kutokana na sakata hilo ni Kangi Lugola, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Rais Magufuli aliwatuhumu viongozi hao kutosimamia masilahi ya nchi wakati wanafanya makubaliano ya mkataba huo baina ya Tanzania na kampuni ya kigeni iliyopewa zabuni ya uuzaji wa vifaa hivyo.

Licha ya kuwaondoa kwenye nyadhifa zao, Rais Magufuli aliagiza mamlaka husika kufanya uchunguzi dhidi ya sakata hilo, ambapo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), ilitekeleza agizo hilo.

Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali, John Mbungo akizungumza na waandishi wa habari tarehe 21 Febriari 2020, alisema baada ya kukamilisha uchunguzi wao na kubaini linahusiana na uhujumu uchumi, watapeleka jalada hilo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka (DPP) kwa hatua zaidi.

error: Content is protected !!