Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli: Msichague wenye kuhubiri chuki
Habari za Siasa

Rais Magufuli: Msichague wenye kuhubiri chuki

Rais John Magufuli akizungumza na Baraza la Kanisa la TAG
Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli amewataka Watanzania kutochagua wanasiasa wanaohubiri chuki na k6utoa maneno ya vitisho. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Kiongozi huyo wa nchi ametoa kauli hiyo leo Ijumaa tarehe 14 Agosti 2020, katika maadhimisho ya miaka 13 ya moto kwenye Mkutano Mkuu wa Kanisa la Assembly of God (TAG) jijini Dodoma.

“Hivyo, nawasihi wanasiasa wenzangu tujipange kufanya kampeni za kistaarabu, tusitumie lugha za kuwatisha wananchi wetu, niwaombe Watanzania tuwakatae wanasiasa wanaohibiri chuki na kutoa maneno ya vitisho,” amesema Rais Magufuli.

Katika kusisitiza hilo, Rais Magufuli amesema “wanafanya hivyo kwa vile hawana sera za kuwaambia wananchi, lakini wanajua vurugu zikitokea wao wanapakwenda kuishi.”

Rais Magufuli amesema, serikali anayoiongoza itahakikisha kwamba uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba 2020, unakuwa huru na haki.

Pia amewataka viongozi wa dini kuhakikisha wanaliombea Taifa ambalo ni miongoni mwa nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Pamoja na kuzungumzia masuala mbalimbali, Rais Magufuli amegusia suala la uchaguzi mkuu akisema, “uchaguzi ni zoezi muhimu katika kupata viongozi kwa njia ya kidemokrasia.”

Amewasihi viongozi wote wa dini nchini kutumia nafasi walizonazo kuhimiza waminini kushiriki katika uchaguzi huo utakaofanyika siku ambayo si ya kusali kwa wamumini wa dizi zote “siku hiyo itakuwa ya mapumziko.”

“Hatuna budi kumwomba Mwenyezi Mungu atupatie viongozi wenye maono, wachapa kazi na wazalendo kwa Taifa letu, tusiangukie mikononi mwa viongozi wabadhirifu, wabinafasi au vibaraka,” amesema Rais Magufuli.

Amesema, kazi ya viongozi kama hao huwa ni kubomoa badala ya kujenga, kung’oa badala ya kupanda na kutawanya badala ya kukusanya “hivyo Mwenyezi Mungu atujalie hekima ili tufanye maamuzi yaliyo sahihi.”

Rais Magufuli amesema, katika baadhi ya nchi, wakati mwingine zoezi la uchaguzi imekuwa chanzo cha kuzuka kwa vurugu na fujo.

“Niwaombe viongozi wa dini kuliombea na kuliweka Taifa letu katika mikono ya Mungu ili tumalize salama uchaguzi na kubaki na amani, umoja na mshikamano kama taifa.”

“Kwangu mimi naliona Taifa la Tanzania muhimu zaidi kuliko mifarakano ya mambo mengine. Napenda kuwathibitishia kama Serikali nilivyoahidi hapo nyuma, tumejipanga kuhakikisha uchaguzi mkuu unakuwa huru na haki,” amesema na kuongeza:

“Sisi kama Watanzania tusimame kama Taifa moja, vyama visitugawe na dini zisitugawe na makabila yasitugawe, sisi tuishi. Nina imani viongozi wa dini wakisimama sisi tutavuka salama,” amesema Rais Magufuli.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!