Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli, Mama Janeth ziarani Malawi
Habari za Siasa

Rais Magufuli, Mama Janeth ziarani Malawi

Spread the love

RAIS John Magufuli leo tarehe 24 Aprili 2019, anatarajia kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Malawi. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa inaeleza kwamba, Rais Magufuli akiambatana na mkewe Mama Janeth Magufuli, wameondoka nchini kuelekea Malawi kwa ajili ya ziara hiyo ya kiserikali.

Taarifa hiyo inaeleza kwamba, Rais Magufuli anafanya ziara hiyo kufuatia mwaliko aliopewa na Rais wa Malawi, Profesa Arthur Mutharika.

“Rais amagufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli ameondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kikataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na atapokelewa rasmi na mwenyeji wake Rais Mutharika,” inaeleza sehemu ya taarifa ya Musigwa.

Katika ziara hiyo, Rais Magufuli anatarajia kutembelea maeneo mbalimbali ya kihistoria nchini Malawi, pamoja na kufungua msimu wa soko la tumbaku na kuzungumza na wadau wa zao hilo.

“Atafanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Mutharika na jioni atahudhuria dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa kwa heshima yake na Rais Mutharika,” inaeleza taarifa ya Msigwa.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, baada ya ziara hiyo kumalizika kesho tarehe 25 Aprili 2019, Rais Magufuli atafanya ziara ya kikazi ya siku nane mkoani Mbeya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!