Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli kufungua shule, amshangaa Spika kuvaa barakoa
Habari za SiasaTangulizi

Rais Magufuli kufungua shule, amshangaa Spika kuvaa barakoa

Spread the love

DK. John Magufuli, Rais wa Tanzania, amesema atafungua shule za msingi na sekondari hivi karibuni, kama ataridhishwa na kasi ya upunguaji wa maambukizi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu, inayosabishwa na virusi vya corona (Covid-19). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Rais Magufuli amesema hayo leo Ijumaa tarehe 5 Juni 2020, wakati akifungua mkutano mkuu wa uchaguzi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), jijini Dodoma.

Amesema, maambukizi ya corona yamekuwa yakipungua siku hadi siku huku akiendelea kuwasisitiza wananchi kuchukua tahadhari  ya ugonjwa huo.

Huku akishangiliwa na umati wa mkutano huo, Rais Magufuli amepiga marufuku usambazaji wa barokoa holela na kuagiza viongozi wa ngazi zote nchini wachukue hatua kwa wale wote wanaozigawa bila kuzingatia utaratibu kutoka wizara ya afya.

“Ukitaka kuvaa barakoa kashone yako, mbona ni rahisi tu,” amesema Rais Magufuli.

Akiendelea kuzungumza, Rais Magufuli amefurahishwa na washiriki wa mkutano huo walioujaza uwanja wa Jamhuri, Dodoma kutokuvaa barakoa huku akionyesha kushangazwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai kuvaa barakoa akiwa ndani ya Bunge.

Rais Magufuli amesema, aliamua kutowafungia watu ndani ‘lockdwon’ kwani kama angefanya hivyo, angewasababishia adha kubwa wananchi ikiwemo kukosa chakula.

“Hapa walimu siwaoni waliovaa sijui ma nini wanavaa mdomoni, sijui ma barakoa, hakuna na hata leo tunaonana tu hapa kawaida na ndiyo maana nilikuwa namshangaa tu Spika akiwa bungeni yuko kwenye kiti peke yake amelivaa hilo li barakoa,” amesema Rais Magufuli.

Huku akishangiliwa, Rais Magufuli amesema,“Tulianza na Mungu na tutamaliza na Mungu, ndugu zangu walimu katoeni elimu hiyo, tutashinda na ndiyo maana mmeona ndege zimeanza kuja, tunaomba watalii waje.”

“Ndiyo manaa sisi hatikuweka lockdown, ukiweka lockdown ina maana hakuna kitu kingekuwa kinafanyika, miradi yote isingekuwa inafanyika, huwezi kwenda shambani na ukishajiweka lockdown umejiua,” amesema Rais Magufuli

Kiongozi huyo mkuu wa nchi amesema, wakati wa shida ndiyo wa kumkimbilia Mungu na si shetani na ndiyo maana katika maombi ya siku tatu yamezaa matunda.

“Nashukuru Mungu na nawashukuru sana Watanzania, tumeshinda na tukaendelee kushinda na mimi nina hakika hivi karibuni baada ya kufungua vyuo, tunaangalia mambo yanavyoenda na shule za msingi na chekechea na nini nazo ziko mbioni tutazifungua ili walimu wa Tanzania wakafanye kazi,” amesema

Tarehe 17 Machi 2020, Serikali ya Tanzania ilitangaza kuzifungua shule zote ikiwa ni siku moja kupita tangu mgonjwa wa kwanza wa corona aliporipotiwa nchini humo. Kesho yake yaani tarehe 18 Machi 2020, vyuo vyote navyo vilifunguwa.

Tarehe 21 Mei 2020, Rais Magufuli wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali aliowateuwa, Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma, aliagiza vyuo vyote na wanafunzi wa kidato cha sita pamoja na michezo, vifunguliwe kuanzia tarehe 1 Juni 2020.

Wanafunzi wa kidato cha sita waliokuwa wafanye mtihani wa mwisho kuanzia tarehe 4 Mei 2020, sasa wako shule kujiandaa na mitihani hiyo itaanza tarehe 29 Juni hadi 16 Julai 2020 na matokeo yakitakiwa kutoka kabla ya tarehe 31 Agosti 2020.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amewataka Watanzania kutotilia maanani baadhi ya maneno ya uongo kutoka kwa watu wa nje, kuhusu milipuko ya ugonjwa mbalimbali.

“Tulizushiwa tukaambiwa tuna Ebola, walijua watalii hawataenda huko, tukasema sisi hatuna Ebola, wala hatuna mjukuu wala hawara yake Ebola, waling’ang’ana tukasema sisi hatuna na kweli hatukuwa na Ebola.”

“Hatukuona mgonjwa amekufa kwa Ebola, hilo likapita, “ amesema Rais Magufuli na kuongeza:

“Umekuja ugonjwa wa Corona walikuwa wanazungumza kwamba maiti zitazagaa kwenye barabara hasa Afrika, wao walikuwa watabiri walishindwa kuelewa Mungu analipenda taifa la Tanzania pamoja na Afrika,” amesema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!