January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli kuanza na kiwanda cha Urafiki

Spread the love

RAIS wa Tanzania John Magufuli ameahidi kusimamia na kuhakikisha kiwanda cha nguo cha urafiki kilichopo Ubungo kinarudi katika ubora wake. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick alipokuwa akihutubia kwa niaba ya rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli katika uzinduzi wa maonesho ya 16 Ujasiliamali wa sekta isiyo rasmi Afrika Mashariki, katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

Kwa niaba ya Rais, Sadick amesema kupungua kwa uzalishaji wa kiwanda hicho kunasababisha ongezeko la kundi la wasio na kazi ambao usababisha kutokuwa na usalama kutokana na wizi.

Amesema kuwa kiwanda hicho kwa sasa kinazalisha mita milioni sita za vitenge na kanga, kwa mwaka, lakini serikali itahakikisha inakirudisha katika uwezo wake wa zamani wa kuzalisha mita milioni 60, ili kuongeza ajira kwa vijana iliyokosekana kwa muda ambao kiwanda hiko kilikuwa hakifanyi kazi.

Sadick amesema kuwa kutokana na serikali kutambua pia umuhimu wa sekta isiyo rasmi, ameagiza manispaa mbalimbali nchini kutangaza maeneo ya kufanyia biashara kwa wajasiliamali wadogo ili kuondoa tatizo la ukosekanaji wa soko kwa wajasiliamali wadogo.

Amesema kutokana na sekta isiyo rasmi kuonekana ni sehemu kubwa ya fulsa ya kujiajiri serikali itahakikisha inaunga mkono katika kutafuta soko na kuwapatia maeneo maalum kwa biashara zao.

“Sekta isiyo rasmi ni muhimu sana katika nchi za Afrika Mashariki kutokana na utoaji wake wa fulsa kwa mwaka 2014, zaidi ya ajira zaidi ya milioni nne,” amesema Sadick.

Sadick amesema kuwa serikali itasimamia upatikanaji wa fulsa za elimu kwa wajasiliamali ili kutatua matatizo ya uelewa wa jinsi ya kujimudu katika biashara mbalimbali pamoja na kukuza kipato kwa kupitia ujasiliamali.

error: Content is protected !!