December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli, Kikwete wateta Ikulu

Rais John Magufuli akiwa na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete

Spread the love

RAIS John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dk. Jakaya Kikwete leo tarehe 23 Oktoba 2018 Ikulu jijini Dar es Salaam. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, inaeleza kuwa Rais Magufuli na Dk. Kikwete wamekutana kwa utaratibu wa kawaida wa kusalimiana na kutakiana heri katika majukumu.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, katika mazungumzo hayo Dk. Kikwete amesifu utendaji kazi wa Rais Magufuli na kumtaka aendelee hivyo hivyo, huku akiahidi kumpa ushirikiano wa hali na mali.

“Nimekuja kumsalimia na kumtakia kila la heri, anafanya kazi nzuri aendelee tu kuchapa kazi na sisi tupo kwa namna yoyote ya kumpa nguvu, tupo tayari kumsaidia,” amesema Dk. Kikwete.

error: Content is protected !!