Friday , 9 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Rais Magufuli, Kikwete waongoza salamu za mwisho kwa Ruge
Habari Mchanganyiko

Rais Magufuli, Kikwete waongoza salamu za mwisho kwa Ruge

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alipokuwa na Marehemu Ruge Mutahaba
Spread the love

RAIS John Magufuli leo tarehe 2 Machi 2019 ameongoza mamia ya watu ikiwemo baadhi ya viongozi wa kiserikali, kuuaga mwili wa Ruge Mutahaba. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Shughuli ya kuuaga mwili wa Ruge, aliyekuwa mtayarishaji wa vipindi vya Clouds Media Group (CMG) imefanyika leo ambapo viongozi wengi wa serikali, taasisi, wasanii na wananchi wengine walipata fursa ya kushiriki kutoa heshima za mwisho kwa Ruge.

Rais Magufuli alikuwa wa kwanza kuuaga mwili wa Ruge katika viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam, akiambatana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa; Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya  Kikwete.

Viongozi wengine walioshiriki shughuli ya kuuaga mwili wa Ruge ni, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Uwekezaji, Angellah Kairuki, Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira, January Makamba na Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba.

Akitoa salamu za rambirambi katika shughuli hiyo, Mwakyembe amesema tasnia ya habari imepoteza mtu muhimu.

“Kwa kile nilichokisikia hapa ndiyo nimefahamu kwa nini tangu nimepata taarifa hizi Watanzania wengi wanabubujikwa na machozi, sababu wanatambua alichokuwa anakifanya. Ruge alikuwa kijana wangu na kiongozi wa tasnia ya habari ambayo ninaiongoza,” amesema Mwakyembe.

Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole, Mbunge wa Mtama na Nape Nnauye na Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule ‘Profesa Jay’ ni miongoni mwa wanasiasa waliohudhuria katika shughuli hiyo.

Vile vile, wasanii wengi walijitokeza kuuaga mwili wa Ruge ambaye katika enzi za uhai wake alishiriki kwa kiasi kikubwa kuinua tasnia hiyo na kuibua vipaji vya wasanii, Ali Kiba, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, Omary Nyemba ‘Ommy Dimpoz’, Abdul Chande ‘Dogo Janja’, Barnaba Elias ‘Baranaba Boy’, Hadija Kopa, Peter Msechu na kikundi cha THT .

Barnaba Boy ameelezea namna marehemu Ruge alivyomsaidia wakati yuko hai akisema kuwa “Ruge kama huna kodi ya nyumba anaenda kukopa anakupa, mama yangu alifariki miaka minne iliyopita Ruge alikuwa baba na mama pia.”

Profesa Jay amesema “Ruge alinifundisha ukiwa na jambo lolote lisimamie na uthubu, leo niko hapa kwa sabahu ya jasiri muongoza njia, thamani ya mtu haitokani na mtu ameishi miaka mingapi, bali ni kutokana na aliyoyatenda.

“Ruge alisimama kusaidia watu na hivyo sisi ili tumuenzi tunedelee kusheherekea maisha yake, wasanii nawaomba tushirikiane kama Ruge alivyotuunganisha.”

Profesa Jay amesema “Ruge alinifundisha ukiwa na jambo lolote lisimamie na uthubu, leo niko hapa kwa sabahu ya jasiri muongoza njia, thamani ya mtu haitokani na mtu ameishi miaka mingapi, bali ni kutokana na aliyoyatenda.

“Ruge alisimama kusaidia watu na hivyo sisi ili tumuenzi tunedelee kusheherekea maisha yake, wasanii nawaomba tushirikiane kama Ruge alivyotuunganisha.”

Baada ya mwili wa Ruge kuagwa jijini Dar es Salaam, mwili wake unatarajiwa kusafirishwa Bukoba mkoani Kagera kesho kwa ajili ya maandalizi ya shughuli ya mazishi yatakayofanyika Jumatatu tarehe 4 Machi

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi zaidi ya 100 wapigwa msasa wa udereva kukabiliana na ajali

Spread the love  KATIKA kuhakikisha wimbi la ajali za barabarani zinapungua kama...

Habari MchanganyikoTangulizi

Serikali yakana kuhamisha kwa nguvu jamii ya Kimasai Loliondo

Spread the loveWAZIRI wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Dk. Damas Ndumbaro,...

Habari Mchanganyiko

Tunduma watenga 60 milioni kujenga machinjio ya kisasa

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma Imetenga kiasi cha Tshs Miloni 60...

Habari Mchanganyiko

Bilioni 17 kujenga bandari kavu Tunduma

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma iliyopo wilayani  Momba mkoani Songwe imepatiwa...

error: Content is protected !!