August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli, Kagame uso kwa uso

Spread the love

RAIS John Magufuli na Paul Kagame, Rais wa Rwanda wamekutana kwenye uzinduzi wa Daraja la Rusumo na kituo cha huduma, anaandika Wolfram Mwalongo.

Uzinduzi huo ambao ni kiungo muhimu kwa maendeleo ya nchi hizo mbili pia umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa ngazi za juu kutoka nchi zote mbili, mabalozi na viongozi wa taasisi za kitaifa na kimataifa.

Akizungumza katika uzinduzi huo Rais Magufuli amewataka wananchi wa pande zote kulinda na kutumia fursa ya daraja hilo kujiletea maendeleo.

Hata hivyo amevitaka vyombo vya usalama kuwachukulia hatua wale wote watakaohusika na uharibifu wa miundombinu hiyo.

Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa ameeleza faida za mradi huo kwamba ni kiungo muhimu cha kunganisha Jumuiya ya Afrika Mashariki na jumuiya nyingine za kikanda kama Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Soko la Pamoja la Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA).

Ujenziwa daraja hilo na kituo cha huduma pamoja mipakani ni moja ya miradi iliyotekelezwa kwa msaada wa Serikali ya Japan kwa Nchi Tanzania na Rwanda kupitia shirika lake la JICA.

error: Content is protected !!