April 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli: Jeshi msikubali vikwazo

Rais John Magufuli

Spread the love

RAIS John Magufuli, Amiri Jeshi Mkuu wa Nchi, ameyataka majeshi nchini kutokubali kuwekewa vikwazo, katika utekelezaji wa majukumu yake. Anaripoti Martin Kamote…(endelea)

Rais Magufuli ametoa wito huo leo tarehe 25 Novemba 2019 wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa, Kikombo, Wilaya ya Chamwino jijini Dodoma.

“Milima yote chukueni ili  mlinde vizuri nchi hii, najua mtaitumia vizuri sababu majeshi ya Tanzania ni imara, msipate vikwazo. Mtu akikaa kule na ng’ombe amewapa vikwazo. Na jeshi halitakiwi kupewa vikwazo, labda vikwazo wakati wa mazoezi, vinavyowafanya kuwa imara, “ amesema Rais Magufuli.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amesisitiza usalama wa viongozi wa jeshi, na kuwashauri makazi yao yasijulikane hovyo.

“Lazima muelewe vitu vingine lazima viwe vyenu, kama ni nyumba anakaa CDF wengine wasipajue, kama ni nyumba anakaa askari wa jeshi wengine si lazima wapajue.

Ninatambua yale yote mliyokuwa mnayaonesha leo, ni mfano wa mtakayoyafanya sio uhalisia,” ameshauri Rais Magufuli.

error: Content is protected !!