NCHI za Afrika hazina nguvu katika soko la kimataifa hasa kwenye malighafi, hupangiwa bei ya kuuza kwa wenye viwanda. Anaripoti Regia Mkonde … (endelea).
Rais John Magufuli ametoa kauli hiyo leo tarehe 5 Agosti 2019, katika Ufunguzi wa Maadhimisho ya Awamu ya Nne ya Wiki ya Viwanda yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
“…na kwa kuwa malighafi hizi hazijaongezewa thamani, tunaziuza kwa bei ndogo sana. Wanunuzi wa bidhaa ghafi, ndio wapangaji wa bei, kwani wasipozinunua hatuana pa kuzipeleka. Mwenendo huu ndio umewadidimiza sana wakulima wetu,” amesema Rais Magufuli na kuongeza;
“Kwasababu ya kutokuwa na viwanda, Nchi za Afrika zimebaki kuwa masikini, tumeendelea kuwa wazalishaji wa malighafi, kwa ajili ya mataifa ya wenye viwanda, na huo ndio ukweli.”
Akizungumza kwenye uzinduzi huo amesema, viwanda ni muhimu katika kukuza uchumi, viwanda na kuwa, ndio njia sahihi katika kukupambana na umasikini pia ukosefu wa ajira.
“Viwanda ndio vilileta utajiri mataifa yaliyoendelea kama Marekani, Japani, Ujerumani, Uingereza na Ufaransa,” amesema.
Amesema, katika miaka ya hivi karibuni, nchi za Asia ambazo kwenye miaka ya 1960 na miaka ya 1970 ziliwiana na mataifa ya Afrika, lakini zimepiga hatua kubwa.
“Nchi za Asia tulikuwa na viwango tunavyoshabihiana kimaendeleo kama vile China, India Korea, Korea ya Kusini, Mlaysia, Thailand, Vietnam lakini nazo zimepiga hatua kubwa kimaendelea kupitia sekta ya viwanda,” amesema.
Amesema kuwa, historia ya mataifa yaliyoendelea inatufundisha kuwa hakuna njia ya mkato kufikia mapinduzi ya kiuchumi na kwamba, ni lazima yapitie kwenye mapinduzi ya viwanda.
Leave a comment