Tuesday , 21 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli hapendi hamahama za wabunge, madiwani
Habari za SiasaTangulizi

Rais Magufuli hapendi hamahama za wabunge, madiwani

Spread the love

WIMBI la hamahama ya madiwani na wabunge wa upinzani nchini limelalamikiwa kuwa linaipeleka nchi kwenye giza la uchumi kutokana na kuingia kwenye gharama za uchaguzi zisizo na umuhimu. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Baadhi ya wabunge na madiwani wa upinzani wamekuwa wakihama vyama vyao kwa madai kuwa wanaunga mkono juhudu za Rais John Magufuli.

Akizungumza na vyombo vya habari leo tarehe 31 Agosti, 2018, Deus Kibamba, Mtafiti wa Jukwaa la Katiba Nchini (JUKATA) amesema kujiuzulu kwa wabunge na madiwani nchini, kunakinzana na jitihada za Rais Magufuli za Tanzania ya viwanda.

Kibamba amesema kuwa, Rais Magufuli hafurahishishwi na vitendo hivi vinavyoigharimu nchi kutokana na marudio ya uchaguzi unaofanyika kila wanasiasa wanapojiuzulu.

Amesema kuwa JUKATA imetoa mapendekezo ya sheria itakayodhibiti vitendo hivi na kuikomboa nchi kwenye shambulio la kiuchumi lililopitia mlango wa kisiasa.

Moja ya mapendekezo hayo ni kutorejea uchaguzi kwa diwani au mbunge atakayejivua nafasi yake ndani ya chama na kuhamia chama kingine na kurejea kugombea kwa chama alichohamia kama inavyofanywa sasa.

Mapendekezo hayo yamehalarisha uchaguzi kurejewa kwa jimbo au kata ya diwani au mbunge aliyefariki pekee.

Kibamba amesema kuwa mapendekezo hayo wanayapeleka bungeni yajadiliwe kisha kwa wananchi ili kuikomboa nchi kwenye gharama zenye kiitia hasara nchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!