June 19, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli: Hakuna demokrasia isiyo na mipaka

Rais John Magufuli

Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli amesema, lengo la demokrasia sio kusababisha vurugu na kwamba, hakuna demokrasia isiyo na mipaka. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Ijumaa tarehe 13 Novemba 2020, Rais Magufuli amesema, uhuru na haki vinakwenda sambamba na wajibu.

“Katika miaka mitano tutaendelea kukuza demokrasia, kulinda uhuru na haki ya wananchi na vyombo vya habari. Hata hivyo, ningependa kukumbusha kuwa lengo la demokrasia ni kuleta maendeleo na siyo fujo na hakuna demokrasia isiyokuwa na mipaka.”

“Uhuru na haki vinakwenda sambamban na wajibu na hakuna uhuru na wajibu usiokuwa na haki vyote vinakwenda sambamba na najua nimeeleweka vizuri,” amesema Rais John Magufuli.

Wabunge wakisikiliza hotuba ya Rais John Magufuli

Rais Magufuli amesema, uchaguzi mkuu wa Tanzania uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020, umetumia asilimia 100 ya fedha za Watanzania hatua inayothibitisha ‘ukomavu.’

Rais Magufuli aliyefika kwenye viwanja hivyo vya bunge saa 3:22 na kukagua gwaride pamoja na kupigia mwimbo wa taifa, ameanza hotuba yake saa 3:57 asubuhi kwa kumkumbuka Hayati Benjamin Mkapa, Rais wa Awamu ya Tatu aliyefariki dunia tarehe 24  Julai 2020 pamoja wa bunbge wengine.

Kwenye hotuba yake Rais Magufuli amesema “uchaguzi ulikuwa wa wazi, amani na utulivu mkubwa na umekwisha, NEC (Tume ya Taifa ya Uchaguzi) imesimamia vizurr uchaguzi kuanzia uandikishaji, urejeshaji wa fomu, usimamizi , upigaji kura na utoaji matokeo,” amesema.

Askofu Josephat Gwajima, Mbunge wa Kawe

Kwenye hotuba hiyo Rais Magufuli amempongeza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Semistocles Kaijage, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dk. Wilson Mahera na maofisa wa tume hiyo kwa kusimamia uchaguzi vizuri.

“Nawapongeza mmetumia fedha mlizopewa vizuri, uchaguzi huu ulitengewa Bilioni 331, tume imetumia  Bil 262. Hii ni ishara nuru ya uadilifu NEC,” amesema.

Rais John Magufuli

Rais Magufuli pia amewashukuru viongozi wa duni kwa kuliombea Taifa kabla na wakati uchaguzi na kuwezesha kumaliza uchaguzi kwa Amani, amewaomba viongozi hao kuendelea kuliombea taifa.

Rais Magufuli aliyeanza hotuba hiyo saa 3:57 asubuhi ameihitimisha saa 5:22 asubuhi.

error: Content is protected !!