March 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli: Dar mtaipenda tu

Spread the love

RAIS John Magufuli amesema serikali yake itabadilisha muonekano wa Jiji la Dar es Salaam kupitia miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu hasa ya barabara na madaraja ya juu. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Rais Magufuli ameyasema hayo leo tarehe 27 Septemba 2018 jijini Dar es Salaam wakati akizindua daraja la Mfugale lililoko maeneo ya Tazara.

Rais Magufuli amesema tayari serikali imetangaza tenda za ujenzi wa barabara kutoka Mbagala ,Gerezani , Kivukoni, Chang’ombe hadi Magomeni yenye kilomita 21 ambapo fedha za ujenzi huo zitatolewa na Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB).

“Tunaibadilisha Dar es Salaam na ndiyo maana tulipokuwa tunabomoa nyumba watu walikuwa wanalalamika lakini ukweli tulizingatia sheria na lengo letu ilikuwa kuipenddezesha Dar es Salaam. Vile vile tunapanua uwanja wa ndege na mambo mengine mengi,” amesema.

Vile vile, Rais Magufuli amesema serikali itajenga madaraja ya juu katika maeneo ya Chang’ombe, Mhasibu House maarufu kama Machinjioni.

Kuhusu uzinduzi wa daraja la Mfugale, Rais Magufuli ameagiza ufungwaji wa taa katika daraja hilo uanze mara moja ili kuzuia matukio ya ajali.

“Ili kupunguza ajali nataka daraja lifungwe kamera na hii kazi ianze mara moja, kama mtatumia mkandarasi kama zawadi ili kama mtu amelewa na kusababisha ajali na kuondoka na gari lake ajulikane ni nani. Ninawaomba hii flyover isiwe sababu ya kupoteza maisha ya watanzania,” amesema.

error: Content is protected !!