January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli azuia mil 250 za wabunge wa CCM

Spread the love

KATIKA hali isiyo ya kawaida, Rais John Magufuli amezuia matumizi ya Sh 250 milioni zilizochangwa na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa ajili ya mchaparo wa kupongezana. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Magufuli aliwataka wabunge hao kutumia fedha hizo walizochanga kwa kuzielekeza katika ununuzi vitanda kwa ajili ya wagonjwa wanaolala chini katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Alitoa kauli hiyo, mara baada ya kulihutubia bunge la 11 tangu alipoapishwa kuwa rais baada ya kumaliza kwa uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba mwaka huu.

Akizungumza kwenye mchaparo huo, Rais Magufuli amesema, anajua wabunge hao walichangishana fedha hizo kwa ajili ya kupongezana kwa kunywa na kula kama walivyozoea kufanya.

Amesema, fedha hizo amezizuia kutoka kwenye Sh. 265 milioni zilizochangwa na wabunge hao ambapo katika hizo aliwataka zitumike Sh. 15 milioni huku Sh. 250 milioni zielekezwe katika kusaidia wagonjwa katika hospitali Rufaa ya Taifa.

“Wabunge nawaomba mniwie radhi mnafanya sherehe tofauti na mlivyozoea mnakunywa maji, mnakunywa juice, wala hamna bia wala wine mlizozoea najua mlichanga pesa zenu zaidi ya Sh. 265 milioni lakini mimi ndiye niliyezizuia.

“Nimesema mtumie Sh 15 milioni kwa ajili ya kupongezana zilizobaki 250 ziende zikanunue vitanda Muhimbili kwa ajili ya wagonjwa wanaolala chini,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli, mara baada ya kuapishwa alifanya ziara ya kushtukiza katika hospitali hiyo na kubaini madudu mbalimbali ikiwemo baadhi ya wagonjwa wakilala chini kutokana na kukosekana vitanda.

Awali katika kipindi cha nyuma wabunge pamoja na watumishi wa bunge walizoea kufanya sherehe ambazo zilikuwa zikisheheni vinywaji vikali vya kila aina huku wananchi wakiwa wakikosa huduma muhimu.

Sherehe hizo zilikuwa zikibarikiwa na Rais wa awamu ya nne pamoja na Spika Spika Mstaafu Anne Makinda.

error: Content is protected !!