RAIS John Magufuli amezikataa kampuni 13 zilizojitokeza kununua korosho ghafi na badala yake ameiagiza Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kutoa fedha za kununua zao hilo, kupitia Jesho la Wananchi (JWTZ). Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).
Akizungumza Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 12 Novemba 2018, Rais Magufuli amesema pamoja na makapuni hayo kujitokeza kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wanaachana na wanunuzi hao kwani watawasumbua, hivyo Serikali itanunua korosho ghafi kwa bei ya Sh. 3,300 kwa kilo, na kuagiza JWTZ) kusimamia mchakato wa ununuzi na usambazaji wa zao hilo.
“Tani 92,000 zimeshanunuliwa, TADB tutanunua kwa 3,300 wakalipwe wakulima kwa kila kilo. Ambayo haijabanguliwa inunuliwe 3,300. JWTZ panga kikosi chako vizuri kila ghala lililoko kule lenye korosho mlinde, jeshi muangalie na walipwe bila kuchelewa, watakapokuwa wanalipwa wasidaiwe chochote, sababu walikuwa wanakopa sio wakakae hapo wakati wanalipwa wawakate hapana,” ameagiza Rais Magufuli.
Rais Magufuli ametoa maagizo hayo baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kueleza kuwa, baada ya serikali kutoa siku nne kwa wanaohitaji kununua zao hilo kujitokeza, kampuni 13 zimejitokeza kununua korosho ghafi.
“Nimeamua yafuatayo, hawa waliojaribu kuleta kwako mapendekezo achana nao hawa watakuja kutuchezea watakwambia wanataka kununua baadae wataanza kuleta masharti na kudelay ‘kuchelewa’ kwa wakulima wetu, wanasema watanunua kwa 3,000 je ikipanda bei ya korosho mwezi wa 12 ‘Desemba, hao wanaoendelea kuja wala wasihangaike kuja, nimeshafunga wala wasihangaike, korosho tunanunua wenyewe,” amesema Rais Magufuli.
Leave a comment