Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli awatega wakuu wa wilaya, mikoa
Habari za SiasaTangulizi

Rais Magufuli awatega wakuu wa wilaya, mikoa

Spread the love

RAIS John Magufuli amewaweka mtegoni Wakuu wa Wilaya na Mikoa walioko katika maeneo yenye migogoro sugu  ya ardhi, akiwataka kusema iwapo wameshindwa kuitatua migogoro hiyo ili awateue wengine. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo tarehe 6 Septemba, 2018 wakati akizungumza na wananchi wa Butiama katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa barabara ya makutano ya Nyamuswa-Sanzate-Nata na Ikoma Gate katika sehemu ya makutano ya Sanzate, iliyofanyika Butiama mkoani Mara.  

“….Ukikaa mahali kukiwa na migogoro mjue mmeshindwa kutawala, kuna polisi, kuna sheria ya ardhi na ya vijiji, mna madaraka haiwezekani mkakaa mahali kukawa na migogoro mpaka watu wanashindwa kulima na mvua imenyesha. Kama mmeshindwa kutatua migogoro mseme mmeshindwa nilete wengine. Haiwezekani nchi hii watu wanagombea mipaka tena wote ni watanzania wanazungumzia lugha moja,” amesema.

Rais Magufuli amesema kuwa, ni aibu kwaTaifa lililosifika kwa kutokuwa na migogoro ya ardhi kutokana na hekima za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, kuwa na migogoro hasa katika mkoa wa Mara aliotoka mwasisi huyo wa Taifa.

“Baba wa taifa alizuia migogoro mingi, taifa hili lilisifika kwa kutokuwa na migogoro mingi kutokana na hekima ya baba wa taifa, Ninawaomba msimwaibishe baba wa taifa kwa kuwa na migogoro mingi.” Amesema na kuongeza.

“Mkoa huu migogoro ya ardhi imekuwa ni tatizo, migogoro kati ya vijiji na vijiji na mtu na mtu. Tusije kuwa na migogoro wakati tunaweza kuimaliza wenyewe. Haiwezekani kuwe na vijiji vina mgogoro ndani ya mkoa mmoja, inabidi tuimalize wenyewe.

“Tusiliingize taifa kwenye ,migogoro hiyo. Ninawaomba wakazi wa Butiama, Bunda na maeneo jirani msigombane, msisubiri viongozi wa nchi wa wilaya au mikoa watatulie migogoro yenu.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

Habari za SiasaTangulizi

CAG aibua madudu halmashauri 10, TANESCO na MSD

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!